Mindblown: a blog about philosophy.
-
Tafakari ya kufikirisha 8/365-2025
Njia bora bora ya kujitambua wewe mwenyewe ni kuangalia kwa umakini kila kitu ambacho kinakuumiza kupitia watu kwa wengine by Kevin Kelly
-
Tafakari ya kufikirisha 7/365-2025
Pale unapojaribu mambo makubwa, kushindwa ni jambo la furaha by Wilfred Peterson.
-
Tafakari ya kufikirisha 6/365-2025
Hakuna ukomo wa kiasi gani kiasi tunaweza kuboresha kwenye kile ambacho tumeanza kukifanya. Hakuna ukomo kwenye ubora au kuwa bora by Kelvin Kelly
-
Tafakari ya kufikirisha 3/365-2025
Namna nzuri ya kutamani kufanikiwa kama wengine ni kuanza na kutamani kujua changamoto walizopitia na namna walivyozitatua. Pia unatakiwa kukumbuka mara nyingi watu huwa hawapendi kuonyesha wakati wanapopitia changamoto ila wanapenda kuonyesha mafanikio hadharani.
-
2/365 -2025
Usikubali kuendelea kutatizwa na jambo ambalo ukweli unaweza kupata msaada. Kuna mambo mengi unayofikiria hayana majibu lakini ukweli ni kuwa yana majibu yake kama ukiamua kutafuta msaada ( kanuni ya Lotus Control )
-
Tafakari ya kufikirisha 1/365-2025
Wote tunaweza kufanya maamuzi lakini mwisho wa siku maamuzi ndiyo huamua aina ya maisha tuliyokuwa nayo , amua kipi unataka kuanza nacho mfululizo mwaka huu mpya 2025 hata kama kwa udogo by Ken Levine
-
Tafakari ya 334/366-2024
Wewe ni zao la kile kitu ambacho unakifanya na siyo kile ambacho unakiona au unachokiamini na wala siyo vile ambavyo umekichagua bali ni vile ambavyo unatumia muda mwingi zaidi.
-
Wazo kuanzisha Mkoba au Saccoss Kwenye Vikundi vya Shule zilizosoma
MIAKA MITANO MAMBO MATANO AMBAYO NIMEJIFUNZA TANGU KUTOA WAZO LA KUANZISHA MKOBA/SACCOS KWENYE VIKUNDI VYOTE VYA SHULE NILIZOSOMA MWAKA 2019. Ndio wakati natoa wazo hili niliona changamoto ya kuchangishana fedha kama za misiba au Ugonjwa vitu ambavyo ni dharura ambazo zinaweza kumtokea mtu yeyote kwa sababu kila kitu ambacho tuko nacho tumepewa kwa muda na…
-
Tafakari ya kufikirisha 333/366-2024
Kukiwa na sauti nyingi zinaongea, wewe sikiliza sauti moja ambayo ina tulivu na ya upole. Hiyo ni thamani kubwa.Kwenye sauti nyingi zenye kelele kuna sauti moja ambayo ina thamani kubwa ukilinganisha na sauti nyingine yoyote. Kwa sababu sauti hiyo ni ya upole na Unyenyekevu, si rahisi kuisikiliza ukiwa kwenye kelele za kundi by Miranda
-
Tafakari ya kufikirisha 331/366-2024
Kufanya kitu bora, fanya kitu hicho. Kufanya kitu kikubwa,fanya kitu hicho, fanya kitu hicho.Siri ya kufanya vitu bora ni kuvifanya vitu hivyo kwa kurudiarudia
Got any book recommendations?