Mindblown: a blog about philosophy.

  • Tafakari ya kufikirisha 180/366-2024

    Maisha ya furaha ni pale unapojua kilicho ndani ya uwezo wako na kilicho nje ya uwezo wako.Ukifuata kauli hiyo hutapata msongo kabisa.Kwa chochote kinachotokea, jiulize je kipo ndani ya uwezo wako, kama ndiyo basi chukua hatua na hakuna msongo.Kama jibu ni hapana, hakipo ndani ya uwezo wako basi unapaswa kukikubali kama kilivyo na kuendelea na…

  • Tafakari ya kufikirisha 179/366-2024

    Ushindi Mkuu kwenye maisha yako, ni kuweza kuwa wewe kwenye dunia ambayo inakazana kukubadilisha uwe kama wengine, uwe vile usivyo wewe ,kuwa wewe kwenye dunia inayokazana kukubadilisha uwe kama wengine ni mafanikio makubwa Mwanafalasafa Ralph Waldo Emerson anatushirikisha jambo hili.

  • Tafakari ya kufikirisha 178/366-2024

    Kimbia mbio zako mwenyewe, Hakuna watu wawili ambao wanafanana kwa kila kitu hapa duniani.Hata mapacha wa kufanana,bado hawafanani kwa kila kitu.Hivyo ulivyo wewe, ni toleo pekee ambalo limewahi kuwepo hapa duniani na hakutakuja kuwa na toleo jingine kama lako. Lakini jamii imekupotosha,imekuwa inakufananisha,kukulinganisha na kukushindanisha na wengine kitu ambacho kimepelekea wewe kushindwa kutambua upekee wako…

  • Tafakari ya kufikirisha 177/366-2024

    Maisha yana namna moja ukipaniki ndio unapigwa; kama uliibiwa ukiwa kijana au kutapeliwa ukiwa mtu mzima, usirudie makosa jifunze kwa makosa uliyopitia kwani kuna hali ya kupaniki ambayo walikuwekea ili waweze kutimiza lengo lao hilo.

  • Tafakari ya kufikirisha 176/366-2024

    Usiogope kufanya kazi kwa ukubwa kwenye kile kinachoonekana kazi ndogo.Kila mara unapofanya ifanye, ifanye kwa nguvu kubwa hata kama ni kazi ndogo Mwandishi Dane Carnigie anatushikirisha jambo hili.

  • Tafakari ya kufikirisha 175/366-2024

    Mafanikio hayahusishi kutokufanya makosa kamwe lakini kunahusisha kutokufanya makosa yale ambayo uliyofanya nyuma kwa mara ya pili.

  • Tafakari ya kufikirisha 174/366-2024

    Mafanikio kwa mwonekano wa nje hayana kitu mpaka uwe na Mafanikio kwa ndani. Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa na ustawi na kuwa vizuri.Mtu ambaye Ana utajiri ndani yake ndie mtu tajiri kuliko watu wote by Robin Sharma.

  • Tafakari ya kufikirisha 173/366-2024

    Baada ya muda wa kazi rasmi unayoifanya kuna muda ambao unaupoteza hapo ndipo kwenye ulevi wako, Ndio hapo ndio kwenye ulevi wako kama ukimaliza shughuli unaangalia mpira mpaka usiku wa manane hapo ndipo kwenye ulevi wako,kama unaenda kupiga umbea na kufuatilia maisha ya watu wengine hapo ndio penye ulevi wako ,kama unapata moja mbili na…

  • Tafakari ya kufikirisha 172/366-2024

    Tofauti kubwa kati ya vile tulivyo na vile tunavyoonekana kwenye jamii, ndio tofauti ya ufanisi wa maisha yetu jinsi yanavyofanya kazi. Na hapo pia ndiyo tunakuwa na furaha kiasi kidogo.Kwa nini? Kwa sababu hakuna furaha utaipata tukiwa tunajisaliti mwenyewe.

  • Tafakari ya kufikirisha 171/366-2024

    Usifanye kitu kwa sababu tu umeshakubali kufanya au umekuwa unakifanya, bali fanya kitu kwa kutathmini kama ni muhimu na sahihi kwako kufanya.Usiogope kuvunja msimamo wako pale mambo yanapokwenda tofauti na ulivyotegemea.

Got any book recommendations?