Mindblown: a blog about philosophy.
-
Tafakari ya kufikirisha 89/366-2024
Sisi ni zao la kile ambacho tunakirudiarudia kufanya.Ubora siyo kufanya bali ni kurudiarudia.Tabia zetu zina madhara makubwa kwenye kufikia yale ambayo tunayaratajia kuyafikia kwa kiasi kikubwa yanatuonesha sisi ni akina nani mwasafalsafa Aristotle anatushirikirisha jambo hili kuweza kuweza kujua tabia ni zao la kutenda na kurudiarudia kufanya vitu.
-
Tafakari ya kufikirisha 88/366-2024
Kuweka juhudi ni sehemu moja muhimu katika mafanikio. Na hilo ndilo eneo pekee ambalo una udhibiti nalo. Kuwa na subira ni eneo jingine muhimu sana kwenye safari ya mafanikio, eneo ambalo wengi huwa wanashindwa na mara nyingi hatuna udhibiti nalo kwenye muda matokeo yatakuja yenyewe kwa wakati.
-
Tafakari ya kufikirisha 87/366-2024
Kitu kinachotuumiza siyo kile kilichotokea bali ni mwitikio wetu kwenye kile kitu kilichotokea.Vitu vinaweza kukuumiza kimwili au kiuchumi na kukupa huzuni. Lakini tabia zetu ndio msingi mkuu hazitakiwi kuumizwa kamwe. Ni ukweli kwamba nyakati ngumu zinaweza kutulazimisha kutengeneza nguvu ambayo iko ndani yetu ili kukabiliana na mambo magumu kwa baadae na kuwapa hamasa watu wengine…
-
Tafakari ya kufikirisha 85/366-2024
Usiamini kila kila kitu unachokihisi.Siyo kila hisia ni za kweli. Usiamini kila kitu kitu unachokifikiria.Kwani siyo kila unachokifikiria ni cha kweli hivyo kwa chochote kile tunapaswa kujifunza zaidi na kukipima kitu hicho kabla ya kufanya maamuzi.
-
Tafakari ya kufikirisha 84/366-2024
Kujiamini siyo kitu ambacho kipo vile vile muda wote; kinabadilika kutokana na uwiano kati ya kufanikiwa na kushindwa. Wote kuna nyakati tulishindwa na kukatishwa tamaa ambapo wakati huo tulipunguziwa uwezo wetu wa kujiamini .Ukikubaliana na hiyo hali hautakata tamaa kwa kila unachojaribu pale unapoona kama hauna uwezo mwandishi John Maxwell anatushirika jambo hilo kuhusu kujiamini…
-
Tafakari ya kufikirisha 83/366-2024
Kama itaishi muda mrefu lazima utafanya makosa.Lakini kama utajifunza kutokana na hayo makosa utakuwa mtu bora.Ni jinsi gani unakabiliana na matatizo na siyo jinsi gani yanakuathiri.Kitu kikubwa ni kutokata tamaa raisi Mstaafu wa Marekani Bill Clinton anatueleza jambo hilo kwa kina kukosea siyo tatizo bali ni sehemu ya kujifunza.
-
Tafakari ya kufikirisha 82/366-2024
Mafanikio yetu, ile hali ya kuridhika na furaha zinategemea uwezo wetu wa kushirikiana na watu wengine, msingi mkubwa wa kushirikiana na watu wengine ni kujiweka wewe katika nafasi yake badala ya kuwaweka kwenye nafasi yao, wafanyie watu kile ambacho wewe ungependa kufanyiwa kuwatia Moyo,kuwakubali,kuwasamehe,kuwasikiliza na kuwaelewa waone watu kama hazina na siyo wanaokupinga, neno sisi…
-
Tafakari ya kufikirisha 80/366-2024
Kile ambacho unawaambia watu wakipitia ndio unapaswa kujiambia pia ukipitia hali hiyo, mfano mtu amepatwa na ugonjwa kuna maneno unamuambia ya kumpa pole nawe ukiumwa unapaswa kujiambia maneno hayo kwanza ili kujikumbusha kuna watu pia wamewahi kupitia hali hiyo, kama mtu akipata na msiba kuna maneno ya Pole ambayo tunayatoa ya faraja ambayo mengine yanatokana…
-
Tafakari ya kufikirisha 79/366-2024
Kama lengo lako pekee ni kuwa na Furaha, hilo ni lengo rahisi kufikiwa; lakini kama lengo ni kuwa na furaha kuliko watu wengine; hilo ni lengo gumu kulifikia kwa sababu mara nyingi tunaamini watu wengine wana furaha kuliko walivyo wao na hiyo furaha mwanafalsafa wa kifaransa Montesquieu anatushirikisha jambo hili kama sehemu ya kujidhibiti na…
-
Tafakari ya kufikirisha 78/366-2024
Vikwazo vingi kwenye maisha utaviondoa baada ya kujua tofauti kati ya mwendo na uelekeo na hapo ndio vikwazo vyovyote utashindana navyo kwa kuwa unajua wapi unaelekea na mwendo uliokuwa nao mwandishi wa mashairi Bill Copeland anatuonesha hilo kwa vitendo na kwa kuchukua hatua kubwa kwenye maisha.
Got any book recommendations?