Mindblown: a blog about philosophy.

  • Tafakari ya kufikirisha 101/366-2024

    Mipaka ambayo tumejiwekea wenyewe ndio inayotuzuia.Siyo kitu cha cha kushangaza kuona rekodi nyingi zinawekwa na watu ambao wanaonekana ni wajinga ambao hawajajiwekea mipaka mfano watu maarufu kama Albert Eisten alikuwa na changamoto ya afya ambayo ilijulikana kama dyslexic ambayo inakuwa inampa changamoto kwenye kusoma na kuandika lakini bado hakukata tamaa na kufanya uvumbuzi mkubwa duniani.

  • Tafakari ya kufikirisha 100/366-2024

    Kama unataka kumkopesha mtu yeyote kwenye maisha, mkopeshe fedha zako, lakini usimkopeshe jina lako, kwa nini ni kwa sababu fedha ni rahisi kurudisha lakini jina ni kazi kubwa kurudisha likipotea.Mara zote tambua thamani binafsi kuliko thamani Mwandishi Shiv Khera anatushirikisha kwenye kitabu cha unaweza kufanikiwa zaidi jambo hili.

  • Tafakari ya kufikirisha 99/366-2024

    Watu wote tunafikiria jinsi ya kuibadilisha dunia lakini watu waliofanikiwa mara zote wanafanyia kazi kubadilika wao wenyewe kwanza kabla ya kwenda kuibadili dunia mwandishi Shiv Khera kwenye kitabu chake cha Unaweza kufanikiwa zaidi anatusititiza jambo hili kwa kina kwamba tunapaswa kubadilika wenyewe kwanza na hapo tutaweza kuleta chachu kwa dunia mzima na jamii kupitia mabadiliko…

  • Tafakari ya kufikirisha 98/366-2024

    Uwekezaji ni kitu chepesi kwa sababu inatutaka sisi tuweke pembeni kiasi fulani cha fedha au muda ili kitu kiweze kukua au kutokea.Lakini Uwekezaji ni kitu kigumu kwa sababu kinapingana na mahitaji ya asili ya Mwanadamu ya kutumia, kufurahi na kujiridhisha mahitaji haraka iwezekanavyo mwandishi Vinod Pottayil anatushirikisha jambo hili kwenye kitabu chake cha uwekezaji.

  • Tafakari ya kufikirisha 97/366-2024

    Hakuna juhudi ambazo zinakwenda bure kwa chochote kile ambacho unakifanya hata kama hauoni matokeo kwa wakati husika kuna wakati matokeo yake utayaona muhimu ni kuendelea kuweka juhudi hata kama kwa hatua ndogo kiasi gani.

  • Tafakari ya kufikirisha 94/366-2024

    Kuna kitu kinaitwa fikra mfadhaiko mfano Watu wajinga wanafikiri kufanya mazoezi ni kitu kisicho na maana.Wakati wakiwa na afya njema wanafikiri ni kitu ambacho hawakiitaji.Lakini wakiumwa,watafanya kwa namna yeyote ile mwandishi Shiv Khera anatushirikisha kwenye kitabu chake unaweza kufanikiwa zaidi.

  • Tafakari ya kufikirisha 91/366-2024

    Matatizo yote tunayokutana nayo yanaangukia kwenye makundi matatu i. ambayo tuna udhibiti nayo ambayo yanahusisha tabia zetu binafsi, ii. Ambayo hatuna udhibiti nayo yanayohusisha tabia za wengine na iii.Ambayo hatuna udhibiti nayo ambayo hatuwezi kufanya chochote ambayo yanahusisha vitu vilivyopita au hali halisi tunayokabiliana nayo kwa muda husika. Njia sahihi ya kukabiliana nayo ni kama…

  • Tafakari ya kufikirisha 90/366-2024

    Kilicho nyuma yetu na kilicho mbele yetu ni mambo madogo ukilinganisha na uwezo wetu mkubwa ambao uko ndani ndani maana wanasaikolojia na wataalamu wanasema pamoja na mambo makubwa ambayo wanadamu wamefanya na ugunduzi bado ni asilimia kumi tu ya uwezo wa ubongo imetumika.

  • Tafakari ya kufikirisha 93/366-2024

    Wakati tukiumwa tunawatafuta madaktari bora wenye upekee, wakati wa kujenga tunawatafuta mafundi bora wenye upekee, wakati wa machafuko watafutwa askari hodari wenye upekee kuongeza. Kitu gani kinawafanya kuwa wa kipekee, ni mtazamo.Mtazamo ni bora kuliko ujuzi,kiwango cha taaluma, mwonekano, ulipozaliwa,mtandao na vitu vinavyoendana na hivyo Mwandishi Shiv Khera anatushirikisha jambo hili kwa kina.

  • Tafakari ya kufikirisha 92/366-2024

    Hakuna urafiki bila kujiamini na hakuna kujiamini kama hakuna uadilifu, ndio maana kwenye urafiki wanasema kukopeshana kunaweza kupoteza urafiki maana yake mtu kama atashindwa kurudisha maana yake amepoteza uadilifu ambapo kutapelekea kukosa kujiamini kwa hiyo urafiki wowote msingi wake mkubwa ni uadilifu mwanafalsafa Samuel anatushirikisha jambo hili katika kudumisha mahusiano yetu.

Got any book recommendations?