Mindblown: a blog about philosophy.

  • Tafakari ya kufikirisha 110/366-2024

    Lazima tuwe na uwiano kati ya familia na marafiki,nyumbani na kazi ,tunachoingiza na tunachotumia, hata sukari kwenye miili yetu vyote kinachozidi au kupungua kina madhara.Vitu mojawapo ya vitu vigumu kuweka kwenye maisha ni hivi hapa chini: – Hisia na Utashi – Mahusiano na kujitoa – Upole na Uimara Ni Vitu ambavyo havifundishwi darasani Shiv Khera…

  • Tafakari ya kufikirisha 111/366-2024

    Kitu kidogo ambacho kimefanyika ni bora kuliko mipango mikubwa. Mipango mizuri pekee haitoshi lazima iendane na vitendo.Tunachofikiria au kuamini ni kitu kidogo. Kitu kinachohesabika ni kile kilichofanyika Mwandishi Shiv Khera anazidi kutukumbusha kwenye kuchukua hatua kwenye kitabu chake Unaweza Kufanikiwa zaidi.

  • Tafakari ya kufikirisha 109/366-2024

    Mara nyingi tumekuwa tukiangalia dunia kwa nje na kusahau kwa ndani.Dunia kwa upande wa ndani ni bora kuliko upande wa nje.Tunaviona vitu siyo vile vilivyo bali sisi tulivyo.Kosa kubwa ni kuona kila kinachotuzunguka na kutojiona ndani yetu Mwandishi Shive Khera kwenye kitabu chake cha unaweza kufanikiwa zaidi anatushirikisha jambo hilo.

  • Tafakari ya kufikirisha 108/366-2024

    Ni bora kuwa na mtu mmoja ambaye anafanya kazi pamoja na sisi ambaye hamasa inatoka ndani yake kuliko kuwa na watu mia moja wanaofanya kazi kwa niaba yetu lakini hamasa haitoki ndani yao.Wale ambao wanafanya kazi na sisi wanavaa uhusika kwenye tunachofanya kuliko wale wanaofanya kwa niaba yetu mwandishi Shiv Khera kwenye kitabu chake cha…

  • Tafakari ya kufikirisha 106/366-2024

    Ufanye Ubongo wako kuwa tupu. Usiwe na Hali yoyote, Umbo lolote kama Maji.Maji yanaweza kutiririka , au kuvunjika baada ya kuwa barafu.Kuwa maji, rafiki hii itakufanya muda wote kuwa tayari kujifunza na kujiona kama hauna unachokijua Mcheza Filamu maarufu wa China Bruce Lee anatushirikisha jambo hili kwenye Nukuu zake maarufu ambazo amewahi kuzituma.

  • Tafakari ya kufikirisha 107/366-2024

    Mara nyingi tumekuwa tukiangalia dunia kwa nje na kusahau kwa ndani.Dunia kwa upande wake wa ndani ni bora kuliko upande wa nje.Tunaviona vitu siyo vile vilivyo bali sisi tulivyo.Kosa kubwa ni kuona kila kinachotunguka na kutojiona ndani yetu sisi wenyewe.

  • Tafakari ya kufikirisha 104/366-2024

    Pamoja na kwamba tunatakiwa kuwa madereca makini, lakini pia tunatakiwa kuwa makini na kujilinda sisi wenyewe kwa madereva ambao siyo makini. Kama hatuendeshi gari tukiwa tumelewa hivyohivyo tunapaswa kujitenga na madereva waliolewa.Hiyo ndio njia ya rahisi ya kujitenga na kuvutwa na hisia.

  • Tafakari ya kufikirisha 105/366-2024

    Ni rahisi kufanya kitu sahihi mara ya kwanza na kila wakati kuliko kuelezea kwa nini hatujafanya na kurekebisha kule kutofanya hapo baada mfano ni rahisi kufanya mazoezi dakika 30 kila siku kuliko kuelezea kwa nini haukufanya pale utakapopata changamoto za kiafya ambazo zingeweza kuepukika kwa zoezi hilo Mwandishi Shiv Khera ametushirikisha jambo hilo kwenye kitabu…

  • Tafakari ya kufikirisha 103/366-2024

    Akili iliyotulia ni bora zaidi kuliko elimu ya juu, sifa za kitaalamu,ujuzi na uzoefu ambavyo viko pamoja. Kinachotakiwa kufanikiwa kwenye maisha ni uwiano kati ya akili na hisia Shiv Khera anasisitiza jambo hilo kwenye kitabu chake cha Unaweza kufanya zaidi.

  • Tafakari ya kufikirisha 102/366-2024

    Utajiri ukipotea hakuna kitu kilichopotea.Afya ikipotea kuna kitu kimepotea .Pale ambapo tabia inapotea kila kitu kinapotea. Huu ni mmoja wa msemo wa kale ambao bado unaishi ambao unatukumbusha kuchukua hatua zaidi kwenye maisha yetu kujali afya na tabia zetu kama msingi wa kuinuka na kutengeneza utajiri hata tukiupoteza.

Got any book recommendations?