Mindblown: a blog about philosophy.

  • Tafakari ya kufikirisha 170/366-2024

    Maisha yana namna moja ukipaniki ndio unapigwa,kama uliibiwa ukiwa kijana au kutapeliwa ukiwa kijana usikubali kutapeliwa ukiwa mtu mzima,usirudie makosa jifunze kwa makosa uliyopitia ili uweze kuchukua hatua zaidi za kukabiliana na ushawishi wa kupata matokeo makubwa kwa kutumia nguvu kidogo.

  • Tafakari ya kufikirisha 169/366-2024

    Haijalishi kitu gani kimetokea kwenye maisha yako, wewe pekee unauwezo wa kukabiliana nacho. Ukitengeneza tabia ya kutafuta jambo chanya kwa kila kitu maisha yako yatafikia mafanikio makubwa.Hii ni moja ya kanuni kubwa zaidi ya kanuni zote za Asili za mafanikio na furaha Mwandishi Darnie Carnigie anatushirikisha jambo hili.

  • Tafakari ya Kufikirisha 168/366-2024

    Kama unajipenda wewe mwenyewe, pia unawapenda watu wengine, Kama unajichukia wewe mwenyewe pia unawachukia wengine,kwa sababu Mahusiano na wengine ni kioo cha vile unavyojiangalia wewe mwenyewe.

  • Tafakari ya Kufikirisha 167/366-2024

    Sisi binadamu tunasukumwa na hisia kuu mbili,tamaa ya kupata na hofu ya kupoteza.Lakini nguvu ya hisia hizo hazilingani, hofu ya kupoteza ina msukumo mkubwa kuliko tamaa ya kupata. Mfano kama ukiambiwa kukamilisha jukumu fulani utaongezwa laki moja utajisukuma kufanya lakini ukishindwa hutaumia sana. Lakini ukiambiwa usipokamilisha jukumu hilo utakatwa laki moja,hapo utapambana uwezavyo. Kupoteza laki…

  • Tafakari ya kufikirisha 166/366-2024

    Sumu ya furaha kwenye maisha ni kujilinganisha na wengine. Haijalishi umepiga hatua kiasi gani,kuna mtu amepiga hatua zaidi yako.Kama unayapima mafanikio yako kwa kuangalia wengine,mara zote utajiona hujafanikiwa.Ili kujenga furaha ya kudumu kwenye maisha yako,jitambue ,jikubali,jithamini na jiamini jinsi ulivyo.

  • Tafakari ya kufikirisha 165/366-2024

    Kama Binadamu tabia yetu ni kuyaambia maisha kutusikiliza kwenye kile ambacho tunakitaka.Lakini maisha hayafanyi kazi kwa njia hiyo. Yanatupa sisi kile ambacho tunakiitaji,ambacho ni bora kwetu ambacho ndio tunahamasa nacho kwa kiasi kikubwa.Maisha yako yatafanya kazi vizuri zaidi pale ambapo ukianza kuyasikiliza maisha yako.Yaache maisha yaamue kuliko kusukuma mto wa maji.

  • Tafakari ya kufikirisha 164/366-2024

    Sumu kubwa ya furaha kwenye maisha ni kujilinganisha na wengine.Haijalishi umepiga hatua kiasi gani, kuna mtu amepiga hatua zaidi yako. Kama unayapima mafanikio yako kwa kuangalia wengine, mara zote utajiona hujafanikiwa. Kama unataka kujenga mafanikio ya kudumu kwenye maisha yako, kamwe usijilinganishe na mtu mwingine yeyote, kwa sababu hakuna anayefanana na wewe hapa duniani.

  • Tafakari ya kufikirisha 163/366-2024

    Usichukulie poa chochote ulichonacho kwenye maisha yako, kwa sababu kuna wengine wengi ambao wangependa sana kuwa na kitu hicho ila hawajapata bahati kama yako. Hivyo shukuru kwa kila zuri lililopo kwenye maisha yako na kwa kufanya hivyo utazidi kuyaona mazuri mengi.

  • Tafakari ya kufikirisha 162/366-2024

    Unyenyekevu ni kutambua kwamba siyo kila kitu kitakuja kwako kwa ambao unaoutaka.Wewe unapanga utakavyo lakini dunia inaenda inavyokwenda,haikuangalii wewe.Unyenyekevu ni kupokea matokeo unayopata na kisha kuyatumia kwa namna ambayo ni bora zaidi. Siyo kulalamika kwa sababu hujapata unachotaka au kukata tamaa kwa sababu matokeo yamekuja tofauti na ulivyopanga,

  • Tafakari ya kufikirisha 161/366-2024

    Kuna tofauti kati ya kupenda kitu na kujitoa. Ukiwa unapenda kufanya kitu unafanya ukijisikia.Wakati ukijitoa kufanya kitu haupokei sababu bali matokeo tu, mfano wewe unataka kufanya mazoezi kila Asubuh ndio matokeo yako hautahangaika na hali ya hewa ,ndio maana unaweza kwenda mkoa wenye baridi ukasema haufanyi mazoezi lakini ukienda barabarani utakuta watu wanakimbia ndio tofauti…

Got any book recommendations?