Mindblown: a blog about philosophy.

  • Tafakari ya kufikirisha 131/366-2024

    Wafanyie watu vile ambavyo unapenda wewe kufanyiwa kama unapenda kutiwa Moyo, kukubalika, kusamehewa, kusikilizwa na kueleweka na wewe wafanyie watu kitu hicho pia by John Maxwell anatushirikisha kwenye kitabu cha Kuwa mtu wa watu,mfano kama mtu amepata tatizo fulani ndio maana unaambiwa ujiambie vile ambavyo umekuwa unawaambia watu hao pia kwenye tatizo kama hilo.

  • Tafakari ya kufikirisha 130/366-2024

    Kwenye kusaka Mafanikio hauhitaji hamasa kutoka kwa wengine. Chukua hamasa ya ndani yako katika kuweka malengo. Malengo ambayo yanakudai kila mara unapolifikia lengo la awali Mwandishi Tom Ruth anatushirikisha jambo hili kwenye kitabu chake cha Strength Finder.

  • Tafakari ya kufikirisha 129/366-2024

    Asili haiwezi kuchengeshwa au kudanganywa. Itakupa mrejesho wa juhudi zako baada ya kulipa gharama za juhudi hizo kama unafanya kitu hauoni matokeo endelea kufanya kuna siku matokeo yatapatikana by Napeleon Hill.

  • Tafakari ya kufikirisha 128/366-2024

    Swali: Una bahati kwa kuzaliwa na kipaji kikubwa cha mchezo wa basketball? Jibu: Kila mtu ana uwezo lakini kipaji (talanta) kinataka kuweka kazi zaidi . Ni moja ya mahojiano ya Mwandishi wa Habari na Nguli wa mchezo wa basketball Michael Jordan kuhusu bahati na kipaji ambapo alikazia kipaji lazima kiendane na kukifanyia kazi.

  • Tafakari ya kufikirisha 127/366-2024

    127/366-2024 ” Ukweli wowote hauna umuhimu kulinganisha na mtazamo kuhusu hicho kitu, kwa kupitia mtazamo ndio unatambulisha mafanikio au kushindwa by Norman Vincent Pearle ,mfano hata kama unauza kitu kizuri kama mtu mtazamo wake ni bei kubwa mtazamo wako ndio utaamua zaidi kuliko ubora wa hicho kitu.

  • Tafakari ya kufikirisha 126/366-2024

    Chochote ambacho tunakifikiria katika ubongo wetu na kuulisha ubongo wetu na kukirudiarudia na hisia kuna siku moja kitakuja kuwa kweli mfano hata matukio ambayo yanatokea kwenye jamii ukifuatilia mtu huyo alikuwa anatamka tamka jambo hilo siku moja analitekeleza kweli Mwandishi Earl Nightingale anatushirikisha jambo hilo.

  • Tafakari ya kufikirisha 125/366-2024

    Kosa kubwa ambalo wauzaji wengi wanalifanya ni kuwataka watu waamini kwa sababu zao, kuliko sababu ambazo zinawafanya wateja wao wenyewe wanunue Mwandishi Brian Tracy anatushirikisha kwenye kitabu chake cha Saikolojia ya Mauzo

  • Tafakari ya kufikirisha 124/366-2024

    Kumshawishi Mteja kwamba atapata heshima au utambuzi wa kipekee akitumia bidhaa au huduma inapunguza upinzani (ugumu) katika bei ya kuuzia Mwandishi Brian Tracy anatushirikisha kwenye kitabu chake saikolojia ya kuuza.

  • Tafakari ya kufikirisha 123/366-2024

    Vitu vikiwa kwenye mwendo vinapunguza mwendo kwa sababu vinakuwa vimechoka hii kanuni za awali ya mwendo by Aristole miaka 2000 iliyopita kabla Newton’s laws uwe .

  • Tafakari ya kufikirisha 122/366-2024

    Chochote unachosema kwa mteja kuhusu bidhaa au huduma yako, chukulia anakuangalia wewe na anasema sasa nifanyaje kuhusu bidhaa yako Mwandishi Brian Tracy anatushirikisha jambo hili.

Got any book recommendations?