Mindblown: a blog about philosophy.

  • Tafakari ya kufikirisha 141/366-2024

    Vitu siyo vibaya kama vile tunavyoviona au kuonekana.Hali ambazo zilitupa huzuni, hizohizo ndio ambazo zilitupelekea kuwa na uimara,nguvu na hekima ambazo tumekuwa nazo by Robin Sharma.

  • Tafakari ya kufikirisha 140/366-2024

    Kwenye jamii zetu, ujinga unaonekana kama ni kitu dhaifu. Ingawaje, wale ambao wanaonesha kwamba hawana ujuzi wa kitu na kufuata maelezo ya kujifunza ndio wanakuja kuona mafanikio zaidi ya wengine ambao wanajiona wanajua by Robin Sharma

  • Tafakari ya kufikirisha 139/366-2024

    Ni rahisi kupinga mwanzoni kuliko mwishoni,ndio maana hata ukianza kufanya kitu mwanzoni lazima utapata ugumu lakini baadae dunia itakupisha mfano ukianza kutengeneza tabia ya kuamka mapema mwanzoni utapata ugumu toka kwenye mwili wenyewe lakini baadae mwili utazoea wenyewe.

  • Tafakari ya kufikirisha 138/366-2024

    Kama unataka kushindwa amini kwenye bahati.Kama unataka kufanikiwa amini kwenye kanuni za vitendo na matokeo, hapo utajitengenezea bahati yako binafsi Mwandishi Shiv Khera anatushirikisha jambo hili.

  • Tafakari ya kufikirisha 137/366-2024

    Wakati Mwingine ni Bora kupoteza na kufanya jambo sahihi kuliko kushinda jambo lisilo sahihi aliyewah kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair anatushirikisha jambo hili kwa kina.

  • Tafakari ya kufikirisha 136/366-2024

    Kuwa Mvumilivu na ishi ukiwa na maarifa kwamba vyote ambavyo unavitafuta vipo jirani kuja kama umejiandaa kwa ajili ya hivyo vitu na tarajia vitu hivyo.Majibu yako yanakuja kuwa na Amani Mwandishi Robin Sharma anatushirikisha kwenye kitabu chake cha Hamasika kila siku.

  • Tafakari ya kufikirisha 135/366-2024

    Furaha haipatikani ukifikia mafanikio fulani.Bali inapatikana pale ukifikiria jambo fulani na kufikiria vitu fulani. Furaha haina kitu cha ziada ya hali ya akili jinsi ulivyoiweka na kutafsiri matukio katika maisha yako Mwandishi Robin Sharma anatushirikisha jambo hili.

  • Tafakari ya kufikirisha 134/366-2024

    Mara zote kumbuka kubishana na kushinda ni kumkatisha tamaa ukweli wa kile mtu ambacho anakiamini yule ambaye unabishana nae.Inauma kupoteza kile unachokiamini,kwa hiyo kuwa mwema hata kama uko sahihi kwa kumuelimisha mtu kwamba upande wako siyo sahihi by Haraki Mwakani mfano ni vigumu kumuaminisha mshabiki ndakindaki kama timu yake ni mbovu”

  • Tafakari ya kufirikisha 133/366-2024

    Njia mojawapo ya kuongeza kujiamini ni kuacha kujilinganisha na watu wengine,kujilinganisha mara zote kunakufanya kuwa na mahitaji ya kutimiza Mwandishi John Maxwell anatushirikisha jambo hili kwenye kitabu chake cha kuwa mtu wa watu.

  • Tafakari ya kufikirisha 132/366-2024

    Ushindi Mkubwa kwa kupiga hatua kwa mtu siyo kile alichopata kutokana na kitu hicho bali ni jinsi gani amekuwa kutokana na ushindi huo Mwandishi John Maxwell anatushirikisha jambo hilo kwenye kitabu chake cha kuwa mtu wa watu.

Got any book recommendations?