Mindblown: a blog about philosophy.

  • Tafakari ya kufikirisha 151/366-2024

    Ukikutana na tatizo litatue Halafu kama una ukweli jinsi ya kufanya maamuzi kulitatua.Usiache kufanya maamuzi ya kulitatua tatizo hilo Mwandishi Dale Carnegie anatushirikisha jambo hilo.

  • Tafakari ya kufikirisha 150/366-2024

    Mafanikio siyo kile unachokiona bali kuna vitu ambavyo viko nyuma ambavyo hauambiwi na waliofanikiwa hawakuambii bali ukifikia hiyo hatua ndiyo watakuambia kwenye kila Mafanikio kuna ugumu nyuma yake ambapo hadithi nyingi za Mafanikio hauwezi kusikia.

  • Tafakari ya kufikirisha 149/366-2024

    Hakuna mtu ambaye anakuwa na masikitiko zaidi ya yule mtu ambaye anatamani kuwa mtu fulani zaidi ya vile alivyo kimwili na kiakili Sam Wood anatushirikisha jambo hili.

  • Tafakari ya kufikirisha 148/366-2024

    Pale unapotafuta kosa kwa watu wengine tafuta kosa ambalo lipo ndani yako na yanafanywa na watu wengine,ukiona makosa yako mwenyewe hauwezi kukosoa watu wengine Mwanafalsafa Marcus Aurelius anatushirikisha jambo hili.

  • Tafakari ya kufikirisha 147/366-2024

    Hakuna mtu yeyote hata awe bora kiasi gani ukipitia changamoto yeyote ile jua kuna watu watafurahi, watu watafurahia na kuweka maneno kama alikuwa anajidai sana au alikuwa anaringa sana au alizidi ni vile watu wameona ni njia rahisi ya kulingana nao ishi maisha yako maana hata watu uliwatendea mema wanaweza kukucheka pia Mwanafalsafa Marcus Aurelius…

  • Tafakari ya kufikirisha 146/366-2024

    Kila kitu tunachopitia kina mchango fulani kwa watu kwenye dunia hivyo kwa kila unachopitia jua kitu hicho kina mchango kwenye dunia na hauna haja ya kusema kwa nini kinapitia kwako, hata kuumwa au kufa kwako kuna mchango unatoa kwa watu wengine mwanafalsafa Marcus Aurelius anatushirikisha jambo hili

  • Tafakari ya kufikirisha 145/366-2024

    Kadri ambavyo unaona kuna jambo liko juu ya uwezo wako na hauwezi kulitatua ndivyo ambavyo utazidi kujiona hauna thamani na utaendelea kukata tamaa. Usikubali kuendelea kutatizwa na jambo ambalo ukweli unaweza kupata msaada. Kuna mambo mengi unayofikiria hayana majiby lakini ukweli ni kuwa yana majibu kma ukiamua kutafuta msaada.

  • Tafakari ya kufikirisha 144/366-2024

    Maisha ni shule ambayo inakuwa ambayo kwa kufikirika imetengenezwa kutupa nafasi ya kujifunza kila somo ambalo tunakiwa kujifunza kwenye mtaala wa maisha yetu kwenye sayari tunayoishi. Tunaishi kwenye nyumba ya shule ya dunia nukuu toka Robin Sharma

  • Tafakari ya kufikirisha 143/366-2024

    Dunia inaendeshwa na wivu. Pale tunapoona wengine wamepiga hatua kuliko wewe, unaingiwa na msukumo wa kuhakikisha unajisikia vizuri. Njia mbili zinazotumiwa ili mtu kujisikia vizuri; kuonyesha wengine hawako sahihi na kufanya ili kupata matokeo makubwa. Wewe tumia njia ya kufanya kwa sababu ndio yenye matokeo bora na yanayodumu. Unapofanya unazalisha matokeo yanayodumu kwa muda mrefu…

  • Tafakari ya kufikirisha 142/366-2024

    Moja ya sheria ya asili ambayo inaendesha dunia ni kwamba ukiweka umakini kwenye vitu usivyovitaka kwenye maisha, unazuia vitu unavyovitaka kuvipata.Kile unachoweka muda mwingi kwenye kitu hicho kinakuwa kwenye maisha yako. Usiweke nguvu kwenye vitu usivyopenda kuliko unavyopenda kwani vitakuingia vitu hivyo bali pambania vile ambavyo unavitaka na vitakuja kwako.

Got any book recommendations?