Mindblown: a blog about philosophy.
-
Tafakari ya kufikirisha 161/366-2024
Kuna tofauti kati ya kupenda kitu na kujitoa. Ukiwa unapenda kufanya kitu unafanya ukijisikia.Wakati ukijitoa kufanya kitu haupokei sababu bali matokeo tu, mfano wewe unataka kufanya mazoezi kila Asubuh ndio matokeo yako hautahangaika na hali ya hewa ,ndio maana unaweza kwenda mkoa wenye baridi ukasema haufanyi mazoezi lakini ukienda barabarani utakuta watu wanakimbia ndio tofauti…
-
Tafakari ya kufikirisha 160/366-2024
Usipoteze muda kutafakari mtu bora anatakiwa kuwaje bali kuwa mtu bora, usipoteze muda mtu mwema anatakiwa kuwaje kuwa mtu mwema watu wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi kutafakari ubora wa kitu badala ya kuchukua hatua mfano kama unaona mtu anapost vitu vya hovyo wewe tuma vitu vya maana badala ya kupoteza muda kulaumu wewe fanya kile…
-
Tafakari ya kufikirisha 159/366-2024
Hakuna makosa kwenye maisha,bali ni masomo. Hakuna kitu hicho kinachoitwa uzoefu hasi, bali ni fursa ya ukuaji,kujifunza na kusonga mbele kwenye safari ya ukomavu. Kutoka kwenye kupambana unapata ujasiri.Hata maumivu yanaweza kuwa Mwalimu bora.
-
Tafakari ya kufikirisha 158/366-2024
Kama binadamu hali yetu ni kutaka kuyaambia maisha ni nini tunakitaka.Lakini maisha hayaendi kwa namna hiyo.Yanatupa sisi kile tunachokitaji,kile ambacho ni bora kwetu ambacho chenye maslahi mapana.Maisha yako yatafanya vizuri zaidi ukianza kuyasikiliza maisha kuyaacha yakuongoze kuliko kusukuma mto by Robin Sharma
-
Tafakari ya kufikirisha 157/366-2024
Kama mtu hawezi kukuzuia kufanya kitu sahihi hawawezi kukuzuia kuwa mtu mwema na kuwa Imara kifikra na matendo kuhusu wengine hivyo mara zote hakikisha unatenda mambo yaliyo mema mwafalsafa Marcus Aurelius anasisitiza jambo hili.
-
Tafakari ya kufikirisha 156/366-2024
Mambo mengi unayofanyiwa kwenye maisha ni yale ambayo unavumilia kile ambacho watu wanakuletea au kukupa mfano mtu akikusemea neno baya na ukamuambia haujajisikia vizuri anaweza asirudie tena lakini usipomuambia anaweza kurudia tena.
-
Tafakari ya kufikirisha155/366-2024
Tone la maji likidondoka mara moja halina maana lakini likijirudiarudia linavunja mwamba,kwa hiyo kitu chochote ukifanya bila kuacha na kurudiarudia kitakuwa na matokeo makubwa baada ya muda kama vile maji yanavyovunja mwamba.
-
Tafakari ya kufikirisha 154/366-2024
Uchovu mkubwa ambao tunakabiliana nao kwa asili unatoka kwenye akili,uchovu hasa wa mwili ni kiasi kidogo hivyo mara zote hakikisha unatunza uchovu wa akili ili uweze kuwa Imara na kuweza kujifunza mara zote by J.A Hadifield
-
Tafakari ya kufikirisha 153/366-2024
Jifunze kuwa mnyenyekevu mara zote kwani hata usipokuwepo itaendelea kuwepo , hata usipokuwepo jua litaendelea kuchomoza Mashariki na kuzama Magharibi.Kwa chochote unachofanya jifunze kuwa mnyenyekevu zaidi na usijipe umuhimu ambao haupo kwa kuona usipokuwepo vitu havitaenda Mwanafalsafa Marcus Aurelius
-
Tafakati ya kufikirisha 152/366-2024
Elimu iliyokamilika ni pale kuna Mabadiliko, kama Elimu haifanyiwi kazi hiyo ni burudani.Kwa Maarifa mapya yoyote unayoyapata hakikisha unayafanyia kazi hasa kwa kiasi kidogo ama sivyo itakuwa burudani ,anza sasa kuyafanyia kazi maarifa yoyote utakayopata na utaona maana ya Elimu hiyo.
Got any book recommendations?