Mindblown: a blog about philosophy.

  • Tafakari ya kufikirisha 191/366-2024

    Je unajua sifamojawapo ya mtu anayejiheshimu, Anatakiwa kulipa madeni yake haraka iwezekanavyo, hatakiwi kununua kitu asichoweza kumudu kwenye kitabu cha mtu Tajiri wa Babiloni tunasisitizwa jambo hili ni mara ngapi umekutana na mtu analalamikia kitu alichonunua kama ni simu inamaliza kifurushi,gari inakula mafuta na vitu vingine ambavyo amenunua mwenyewe ndio maana kitu chochote kabla ya…

  • Tafakari ya kufikirisha 190/366-2024

    Tunaweza kujikwaa na kuanguka lakini tunaweza kusimama tena; hiyo itakuwa inatosha kama hatutakimbia kwenye mpambano na kuendelea kung’ang’ana Mahatma Gandhi anatushirikisha Nukuu hii kuhusu kuendelea kuchukua hatua.

  • Tafakari ya kufikirisha 189/366-2024

    Maisha ni kama kupika kinachotakiwa ni kuanza tu vitu vingine vitajiunga vyenyewe kama vile kwenye mapishi kile chenye upungufu kama chumvi na viungo vingine vinaongezwa kadiri mapishi yanavyoendelea hivyohivyo kwenye maisha maarifa yeyote unayopata muhimu ni kuanza.

  • Tafakari ya kufikirisha 188/366-2024

    Kila mtu anaweza kuwa na Hasira, ni kitu rahisi, lakini kuwa na mtu sahihi na wakati sahihi na lengo sahihi na kwa uelekeo sahihi hiyo haipo kwenye uwezo wa kila mtu na siyo kitu rahisi Mwanafalsafa Aristotle anatushirikisha jambo hili.

  • Tafakari ya kufikirisha 187/366-2024

    Ukijilinganisha siku zote utakosa furaha, kwenye kila kitu unachofanya siku zote kuna watu watakuwa wamekuzidi kitu cha msingi cha kuangalia ni kujilinganisha wewe wa jana na leo kwenye chochote unachofanya au kuwa nacho lazima utakutana na mtu amekuzidi mfano ukiwa na baiskeli utakuta watu wanapikipiki,ukiwa na pikipiki utatamani gari,ukifika kwenye gari na utakuta watu wana…

  • Tafakari ya kufikirisha 186/366-2024

    Moja ya sheria ya asili ni hii: Hatupati zaidi ya kile tunaweza kuhimili.Njia ya upendo ambayo imepangwa kwa ajili yako hauwezi kupata maarifa au ukweli zaidi ule ambao uko tayari kuupokea. Kwa hiyo chochote kile kinachokuja kwako pale ambapo upo tayari kukipokea. Mwanafunzi lazima awe mvumilivu. Muda ni kitu muhimu na majibu yatakuja

  • Tafakari ya kufikirisha 185/366-2024

    Fanya kitu sahihi. Fanya kwa njia ambayo inaendana na tabia yako. Fanya kwa uadilifu. Ongozwa na Moyo wako.Vitu vingine vyote vitajipanga vyenyewe Mwandishi Robin Sharma anatushirikisha jambo hili.

  • Tafakari ya kufikirisha 184/366-2024

    Kitu kilichopita ni kama pango na inakuwa haina maana kutumia maisha yako kuishi kwenye pango. Kila mwisho unaashiria mwanzo mpya au kuanza kwa njia nyingine, hauwezi kwenda mbele kwenye maisha au mwendo kama unabaki na kuangalia kioo cha nyuma.

  • Tafakari ya kufikirisha 183/366-2024

    Mtu mwema ni yule anayefanya jambo sahihi, na kuendelea kufanya jambo jingine sahihi badala ya kutangaza kwamba amefanya jambo zuri. Kama ambavyo nyuki hawatangazi wametengeneza asali tamu,tunapaswa kufanya wema siyo kwa ajili ya kuonekana au kujitangaza,bali kwa sababu ndiyo maisha tuliyochagua kuishi.

  • Tafakari ya kufikirisha 182/366-2024

    Kila kitu tunachopitia kina mchango fulani kwa watu kwenye dunia, hivyo kwa kila unachopitia jua kitu hicho kina mchango kwenye dunia na hauna haja ya kusema kwa nini kinapitia kwako, hata kuumwa kwako au kufa kwako kuna mchango unatoa kwa watu wengine Mwanafalsafa Marcus Aurelius anatushirikisha jambo hili.

Got any book recommendations?