Mindblown: a blog about philosophy.
-
Tafakari ya kufikirisha 201/366-2024
Haijalishi wengine wanaona nini,wewe kwenye kila hali na jambo ona fursa zaidi. Hata kama ni kitu ambacho wengine wanaona ni kibaya au kigumu,wewe ona fursa za kuweza kukitumia kwa manufaa zaidi. Hakuna kisichokuwa na fursa ndani yake,unapochagua kuzitafuta na kuwa tayari kuzitumia utaziona
-
Tafakari ya kufikirisha 200/366-2024
Furaha haitokani na kufikia mafanikio fulani. Bali inatokana na kufikiria mawazo fulani na kujisikia hisia fulani. Furaha siyo kitu kikubwa bali ni hali ya akili ambayo watu wanaitengeneza na kuitafsiri mfano unaweza kukutana timu fulani haijapata mafanikio ya kuchukua kombe wakafurahi kupiga chenga au mchezaji wao kafunga goli wamechagua kitu cha kuwapa furaha kwa tafsiri…
-
Tafakari ya kufikirisha 199/366-2024
Hauwezi kubadilisha dunia yako ndani ya siku moja.Anza kidogo kidogo. Hatua elfu moja za safari zinaanza kwa kuchukua hatua ya kwanza. Tunakuwa kikubwa kwa kutumia hatua ndogo ndogo sana. Hatua ndogo ndogo kila siku zinapelekea matokeo makubwa baada ya muda.
-
Tafakari ya kufikirisha 198/366-2024
Mahitaji ya msingi kabisa ya maisha ni rahisi kupata, Chakula, Malazi na Mavazi,lakini pale tunapotaka vitu hivyo vile anasa,viwe kwa ajili ya kuonekana na siyo kwa ajili ya kuishi,hapo ndipo maisha yanapokuwa magumu. Kwa mfano unavaa nguo kwa ajili ya kujisitiri,hutajali sana nguo gani unavaa,lakini pale unapovaa kwa ajili kuonekana na wengine ndipo unapoanza kujitesa…
-
Tafakari ya kufikirisha 197/366-2024
Ukomavu au Ukuaji wa Binadamu ni kupenda kile ambacho uko nacho tayari kuliko kuwa na wasiwasi kuhusu kile unachotamani na kukipenda kuwa nacho.
-
Tafakari ya kufikirisha 196/366-2024
Chochote ulichojenga kwa kuwa wewe,kitaanguka vibaya pale utakapoacha kuwa wewe na kushawishika kuwa vile wengine wanavyotaka uwe. Na hivyo wanaokuzunguka na jamii wanataka uwe, namna wanavyotaka wao,pambana na kukataa hilo,ni vita utakayopigana maisha yako yote .
-
Tafakari ya kufikirisha 195/366-2024
Kama mtu anaweza kunishawishi na kunionesha kwamba nimekosea,nitafurahi na kuwa tayari kubadilika.Ukweli haujawahi kumuumiza yeyote, bali ujinga na kung’ang’a na mazoea kumeumiza wengi Mwanafalsafa Marcus Aurelius anatushirikisha jambo hili.
-
Tafakari ya kufikirisha 194/366-2024
Tumia muda mwingi kujifunza na kuwa mtu bora kitu ambacho kitakupelekea kutokuwa na muda wa kukosoa watu wengine kwenye vitu ambavyo hata wewe hauna ubora huo au uwezo wa kuvifanya Mwandishi Shiv Khera anatushirikisha jambo hili.
-
Tafakari ya kufikirisha 193/366-2024
Hakuna makosa kwenye maisha,bali ni kujifunza. Hakuna kitu ambacho kinaitwa uzoefu hasi, bali ni fursa ya kukua,kujifunza na kuelekea umahiri binafsi kwenye barabara ya kuwa imara. Kutoka kwenye kujitafuta na kuwa imara.Hata maumivu yanaweza kuwa mafundisho tosha Mwandishi Brian Tracy anatushirikisha jambo hili.
-
Tafakari ya kufikirisha 192/366-2024
Matendo ya hekima hutufuata maisha yetu yote. Hutuburudisha na kutusaidia. Hivyohivyo, matendo yasiyo na hekima hutufuata ili kutuumiza na kututesa. Sehemu kubwa ya mateso hayo huwa ni majuto juu ya mambo tuliyopaswa lakini hatukufanya.Majuto juu ya fursa zilizotutembelea lakini tukazipuuza.
Got any book recommendations?