Category: Uncategorized
-
Tafakari ya kufikirisha 298/366-2024
Kama hauwezi kutengeneza tabia ya kuweka akiba ukiwa na kipato kidogo kamwe hautaweza kuweka akiba ukiwa ukianza kupata kipato kikubwa zaidi, msingi mkuu wa kwanza ni tabia kabla ya kipato, Anza na msingi wa tabia na utakuwa imara by Ankur Warikoo
-
Tafakari ya kufirikisha 220/366-2024
Kama mtu akicheka wazo lako, ni kiashiria kwamba ni wazo bora. Kama una wazo au kitu kikubwa ambacho, ukikifanya kitafanya maisha yako kuwa bora, lakini watu wakakucheka, wakakuambia huwezi au haiwezekani, hicho ni kiashiria kwamba wazo bora. Hivyo hakikisha unalitekeleza licha ya wengine kushindwa kuona ubora wake Nukuu toka kwa Jim Rogers
-
Tafakari ya kufikirisha 219/366-2024
Jitoe kwenye kile unachopenda kwenye maisha. Je mtu anaweza kufanikiwa kwenye maisha? Jibu ni rahisi, kujaribu mambo mengi mapema, kujua yale ambayo anayapenda,kisha kuweka nguvu zake zote kwenye yale anayopenda kufanya. Chochote unachopenda kweli, kisha ukaweka maisha yako yote kwenye hicho unachopenda, lazima utafanikiwa, hata kama hutakuwa na fedha nyingi Nukuu toka kwa Jim Rogers.
-
Tafakari ya kufikirisha 218/366-2024
Watu wengi hujitoa sana pale wanapowasaidia wengine, lakini inapokuja kwao binafsi wanapuuza. Mifugo yako ikiumwa haraka utaitafutia matibabu na kuhakikisha inapata matibabu na kuhakikisha inapata matibabu, lakini wewe ukiumwa huhangaiki sana hata ukipewa dawa hutumii kwa umakini kama unavyoelekezwa.
-
217/366-2024
Njia mojawapo ya kuongeza kujiamini ni kuacha kujilinganisha na watu wengine, kujilinganisha mara zote kunakufanya kuwa muhitaji. Kujiamini siyo kitu ambacho kipo vilevile mara zote kinabadilika kutokana na uwiano kati ya kufanya na kushindwa uwe .
-
Tafakari ya kufikirisha 216-2024/366
Usifurahie au Usisherekee matokeo makubwa ambayo hayatokani na wewe usijipe umiliki wa vitu ambavyo vipo nje ya uwezo tofauti kati ya matokeo na mafanikio, mafanikio ni matokeo yanayojirudiarudia wakati matokeo ni kitu matokeo ni kitu ambacho kinaweza kujitokeza mara moja na kisirudie tena by Epictetus.
-
Tafakari ya kufikirisha 215/366-2024
Kabla hujasumbuka na maoni ambayo wengine wanayatoa,Angalia kwanza wao wenyewe wako wapi. Kama wako chini ya maoni hayo, watakatisha tamaa kwa sababu mara zote wanakuwa na maoni hasi. Kama wapo juu, watatia moyo kwa sababu wao wanakuwa wameshafanya. Usiwasikilize watu bila kujua maoni yao yanatokea chini au juu by Dr. Makirita Amani. Mfano mtu ambaye…
-
Tafakari ya kufikirisha 214/366-2024
Kila kitu kinaweza kuondolewa kwa mtu isipokuwa kitu kimoja; uhuru wa mwisho wa mwanadamu- mtu kuchagua mtazamo wa kuwa nao kwa yale anayopitia, mtu kuchagua njia yake mwenyewe by Victor Franklin.
-
Tafakari ya kufikirisha 213/366-2024
Kila mtu anaweza kukosoa, kila mtu anaweza kutoa maoni yake namna gani mambo yanaweza kwenda vizuri, lakini kila mtu kuna kitu ambacho hafanyi kwa usahihi kwenye maisha yako. Kabla hujapoteza muda wako kuhukumu au kukosoa wengine, hebu kwanza angalia maisha yako badala ya kukosoa wengine.
-
Tafakari ya kufikirisha 212/366-2024
Linda muda wako. Jifunze kusema Hapana. Kuwa na ujasiri wa kusema hapana kwenye vitu vidogovidogo kwenye maisha ambayo itakupa nguvu ya kusema Ndiyo kwenye vitu vikubwa pia.