Category: Uncategorized
-
Tafakari ya kufikirisha 321/366-2024
Haichukui nguvu kubwa kufanya vitu, lakini inahitaji nguvu kubwa ya kuamua kitu gani cha kufanya by Elbert
-
Tafakari ya kufikirisha 320/366-2024
Haiitajiki nguvu kubwa kufanya vitu, lakini inahitajika nguvu kubwa kwenye kuamua kitu gani cha kufanya pale ambapo kunakuwa na machanguo mengi by Elbert
-
Tafakari ya kufikirisha 319/366-3024
Kama una lengo basi liandike.Usipoliandika basi hauna lengo bali una matamanio. Chochoteambacho unafikiri hakiwezi kuwa lengo mpaka kiwe kimeandikwa na kukaa kwenye mpango kazi na hapo ndio malengo yanahesabika by Steve Maraboli
-
318/366-2024
Mabadiliko madogo ya namna unavyofikiri yanaweza kupelekea Mabadiliko makubwa kwenye matokeo ya mwisho .Hivyo kwa chochote unavyotaka kufanya huhitaji kuanza na mabadiliko makubwa sana bali hata kubadili kauli chanya unazotamka zinaweza kuvutq fursa kuelekea mabadiliko,jitamkie tu hata neno wewe mshindi au mtu mwenye mafanikio na utaona unaanza kupata ushindi mdogo mdogo kuanzia hapo ulipo by…
-
Tafakari ya kufikirisha 317/366-2024
Usiminye ndoto zako zifanane na uhalisia wa sasa, kama unaona una kitu kikubwa unaweza kukifikia au una jambo kubwa unaweza kulifanya zaidi ya mazingira yanayokuzunguka wewe endelea kuweka msimamo usiache hiyo ndoto yako kwa kuangalia mazingira au watu kwa kuangalia hali ya sasa . Baada ya muda kitu hicho kitakuja kufanya kazi by Jim Kwik
-
Tafakari ya kufikirisha 316/366-2024
Mambo yaliyopita ni kama maji chini ya daraja na mambo yajayo ni kama umbali kati ya miale ya jua na fikra zako.Wakati muhimu sana ni sasa. Jifunze kuishi wakati uliopo sasa na utumie wote bila kujibakisha by Grant Cardone
-
Tafakari ya kufikirisha 315/366-2024
Jilinganishe na ulivyokuwa jana, siyo kujilinganisha na wengine walivyo leo. Kosa kubwa unaloweza kufanya kwenye maisha yako, ni kujilinganisha na mtu mwingine yeyote, awe yupo juu yako,chini yako au sawa na wewe. Mtu pekee wa kujilinganisha naye ni wewe mwenyewe, kama leo umefanya kwa ubora kuliko jana unapiga hatua,kama umefanya kama jana unarudi nyuma,kama umefanya…
-
Tafakari ya kufikirisha 313/366-2024
Kuna watu wanajifunza kutokana na makosa ambayo wamefanya watu wengine. Hawa ni watu wenye busara.Kuna watu wanafikiri kujifunza kwa kweli kunatokea kwa uzoefu wa mtu pekee. Watu kama hao wanavumilia maumivu ambayo siyo ya lazima na msongo kwenye maisha yao yote by Grant Cardone
-
Tafakari ya kufikirisha 312/366-2024
Hakuna kitu ambacho kinatokea kwenye maisha yetu kina maana tofauti na maana ambayo tunaitafsiri. Machungu na maumivu yanatokana na tafsiri zetu. Tukiacha kutafsiri hali tunazokutana nazo kama ni hali chanya au hasi na kuzikubali kama fursa kuelekea kwenye mambo makubwa maisha yetu yanabadilika. Na hapo tutaweza kuwa na Amani na furaha nukuu na Grant Cardone
-
311/366-2024
Watu waliofikia mafanikio makubwa wanalenga nguvu zao kwenye lengo moja na wakishalitimiza wanaenda kwenye lengo lingine. Sheria ya kwanza ya mafanikio ni uwezo wa kupeleka nguvu zako za kimwili na kiakili kwenye tatizo moja bila ya kuchoka nukuu hii ya Thomas Edson inatupa nguvu ya kuchukua hatua zaidi.