Category: Uncategorized
-
Tafakari ya kufikirisha
Kuweka juhudi ni sehemu moja muhimu katika mafanikio. Na hilo ndilo eneo pekee ambalo una udhibiti nalo. Kuwa na subira ni eneo jingine muhimu sana kwenye safari ya mafanikio, eneo ambalo wengi ndiyo huwa wanashindwa. Kwenye chochote unachofanya, kama juhudi unazoweka ni sahihi, unahitaji ni subira tu, hakuna kingine chochote.
-
Tafakari ya kufikirisha
Kamwe usifikirie vitu ambavyo huvitaki, utakaribisha hivyo zaidi. Unachopaswa kufanya ni kufikiria vile tu unavyotaka, fikra zako zitawaliwe na hilo na utaziona fursa nyingi zaidi
-
Tafakari ya kufikirisha
Kujua kwamba mabadiliko yatatokea, kujiandaa kwa ajili ya kunufaika na mabadiliko kutakuletea faida ambapo utaweza kuchukua hatua haraka kabla nafasi ya mabadiliko haijakwisha.Wakati wa kufanya mabadiliko unahitaji kujiamini sana vinginevyo unaweza kuogopa na kubaki nyuma
-
Tafakari ya kufikirisha -02-2024
Pale unapoona watu wamepiga hatua fulani kwenye maisha yao, siyo kwa sababu ndiyo wamekuwa bora kuliko walivyokuwa huko nyuma.Bali wanakuwa fursa ya kudhihirisha uwezo mkubwa ambao tayari upo ndani yao. Ni asili ya Binadamu kwamba watu huwa hawabadiliki.Hivyo chochote unachokiona kama mabadiliko kwa mtu, ni anakuwa tu amechoka kuigiza na kuamua kuwa halisi kwao.Kumbuka hili…
-
Tafakari ya kufikirisha
Ukishapata ushindi kila mtu atakusifia na kusema una akili nyingi.Kila mtu atapenda kujifunza kwako.Lakini kabla ya ushindi,utaonekana huna lolote.Hivyo basi, usiache mpaka umepata ushindi unaotaka kuupata, hata kama hakuna anayekuelewa.Endelea kuvumilia na kupambana, ushindi utakaoupata utafuta yote unayopitia sasa.Ukiweza kuziba masikio yako na kuweka juhudi mpaka upate ushindi, utaweza kufanya makubwa sana nukuu toka Dr.…
-
Tafakari ya kufikirisha
Njia pekee ya wewe kuwa na furaha kwenye maisha, ni kujua vitu gani unajali, kisha kuvifanya kwa ubora wa hali ya juu sana.Kila mmoja wetu kina vitu ambavyo anavijali zaidi kwenye maisha. Kwa wengine inaweza kuwa kazi au biashara, wengine mahusiano yao, wengine eneo fulani la kazi, wengine kuwasaidia watu, wengine kuishi kulingana na falsafa…
-
Tafakari ya kufikirisha
Mwandishi Nguli Robert Kiyosaki Anasema mara nyingi amekuwa akiulizwa Ardhi na Majengoni Uwekezaji bora?Hisa na vipande ni uwekezaji bora? Na jibu lake huwa Hakuna Uwekezaji Salama. Bali kuna Wawekezaji makini. Je wewe ni mwekezaji bora? Hakuna uwekezaji bora kama wewe ni mjinga,hata kwenye dhahabu.Unaweza kupoteza fedha kwa kufanya uwekezaji hata kwenye dhahabu na shaba. Mara…
-
Tafakari ya kufikirisha
Hamasa inaanza na matamanio, hasa ya nje, yanayochochewa na wengine.Lakini nidhamu inaanza na hasira ambazo mtu anakuwa nazo, kwa mabadiliko yanayotakiwa kufanyiwa kazi.Nidhamu huwa inajengwa kwa matendo madogo madogo yasiyokuwa na madhara yoyote.Kadiri unavyokuwa unafanya kwa juhudi kubwa chochote unachokuwa umepanga, ndivyo unavyozidi kuimarisha nidhamu yao ya ufanyaji.
-
Tafakari ya kufikirisha
Makosa makubwa mawili ambayo watu wengi wanayarudia rudia kwenye maisha ni kutokufanya kabisa au kukata tamaa baada ya kufanya na kukosea.Njia ya kuvuka makosa hayo ni kufanya kwa mwendelezo bila kuacha.Kila unapofanya unajitathmini na kuangalia wapi pa kuboresha zaidi unapofanya tena.Ukienda hivyo kwa muda mrefu, utayafuta makosa mengi na kuishia kuwa bora zaidi Nukuu toka…
-
Tafakari ya kufikirisha
Watu huwa wana tabia ya kujaribu kuvuka mipaka uliyoweka ili kuona utachukuliaje hilo.Hivyo kama hujaweka mipaka imara na kuweka madhara pale mtu anaposhindwa kuizingatia, fujo zinakuwa nyingi sana.Hakuna chochote kikubwa kitakachoweza kufanyika kwa kila mtu kujiamulia vile anavyotaka yeye mwenyewe.Ukiwaruhusu watu kuvuka mipaka uliyoweka, hata kama ni kidogo tu, wataenda zaidi ya ulivyowaruhusu.Na hapo unakuwa…