Category: Uncategorized

  • Tafakari ya kufirikisha 31/366-2024

    Hauwezi kuwa mjasiriamali uliyefanikiwa kama hauko tayari kupoteza uwekezaji wako. Kama mradi wako umekufa, usione kama umefunikwa na wingu. Cheka kwa huko kushindwa, na jifunze kwenye makosa. Ni sehemu muhimu ya mchezo. Wakati mwingine utakuwa bora zaidi nukuu toka Strive Masiyiwa Kwenye Nukuu hii Bilionea Strive Masiyiwa anasisitiza kwenye kuchukua hatua kwenye kuanza na kama…

  • Tafakari ya kufikirisha 29/366-2024

    Maisha yatawaumiza baadhi ya watu kwa namna fulani na kuwasaidia wengine. Unapaswa kuwa tayari kupokea mapigo ya maisha kama yanavyokuja. Hivyo ndivyo maisha yalivyo na siyo kulalamika muda wote, kwani kulalamika ni moja ya kitu ambacho kinachukua nguvu zetu zaidi na kuwapa wengine ukuu wetu.

  • Tafakari ya kufikirisha 30/366-2024

    Usitamani watu wawe tofauti bali tamani wajidhihirishe mapema. Usitamani watu wawe vile unavyotaka wewe, bali tamani kuujua uhalisia wao. Ni pale watu wanapokuonyesha uhalisia wao usiwakatalie kutaka wawe tofauti wala usiumie kwa sababu ulitaka wawe tofauti. Unachopaswa ni kupima, kwa uhalisia ambao unaujua kuhusu watu, je bado unaweza kwenda pamoja na kila mtu akanufaika.

  • Tafakari ya kufikirisha 28/366-2024

    Mabadiliko yanazalisha watu wa aina tatu, mabadiliko lazima yatokee na kwa vyovyote vile mabadiliko yanaacha athari ambazo zinaweza kuwa chanya au hasi. Mabadiliko yoyote huzalisha makundi matatu ya watu, makundi hayo ni watu watu wanaonufaika na mabadiliko yoyote, watu ambao wanaamshwa na mabadiliko na watu ambao wanaachwa na mabadiliko.Kwa mabadiliko yoyote tathmini umeangukia kwenye kundi…

  • Tafakari ya kufikirisha 27/366-2024

    Mafanikio na kufanya ni vitu ambavyo vinakwenda pamoja na haviwezi kutenganishwa. Tangu mtu anapoanza mpaka anafanikiwa, lazima awe anaendelea kufanya bila ukomo.Ni kupitia kufanya mtu anapiga hatua kubwa sana kuliko kupanga na kusema pekee. Unachotaka na uchofanya vinapaswa kwenda pamoja ili uweze kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

  • Tafakari ya kufikirisha 26/366-2024

    Chochote unachokifanya kiwe kizuri au kibaya kinatumia nguvu ileile hivyo kwa Chochote unachofanya hakikisha unafanya kizuri maana nguvu unazotumia kufanya ni kwa kutumia muda uleule ambao upo nao kwa wakati husika.

  • Tafakari ya kufikirisha 25/366 -2024

    Msukumo unaotoka ndani ya mtu ndio unaomfanya mtu kuchukua hatua mara moja kwenye kila linalotokea, bila ya kusubiri kwa muda mrefu. Wenye msukumo wa ndani hawasubiri mpaka wapate taarifa zaidi na kujadiliana na wengine ndiyo wachukue hatua.Wao huchukua hatua mara moja pale inapohitajika kufanya hivyo, bila ya kusitasita. Ni msukumo huo wa kuchukua hatua na…

  • Tafakari ya kufikirisha 24/366

    Msukumo unaotoka n dani ya mtu ndio unaomfanya mtu kuchukua hatua mara moja kwenye kila linalotokea, bila ya kusubirii kwa muda mrefu. Wenye msukumo wa ndani hawasubiri mpaka wapate taarifa zaidi na kujadiliana na wengine ndiyo wachukue hatua. Wao huchukua hatua mara moja pale inapohitajika kufanya hivyo, bila ya kusitasita. Ni msukumo huo wa kuchukua…

  • Tafakari ya kufikirisha 23/366-2024

    Wakatishaii tamaa wengi wana nia njema sana na wewe. Wanapokukatisha tamaa usifanye kitu, sio kwamba wanaona wivu ukikipata utakuwa umewazidi, japo kuna wa aina hiyo, bali wanaona unachokwenda kufanya kitakuumiza sana. Hivyo wanavyokukatisha tamaa ni kama wanajaribu kukulinda ili usiingie kwenye matatizo makubwa.

  • Tafakari ya kufikirisha 22/366-2024

    Kadri ambavyo unaona kuna jambo liko juu ya uwezo wako na hauwezi kulitatua ndivyo ambavyo utazidi kujiona hauna thamani na utaendelea kukata tamaa. Usikubali kuendelea kutatizwa na jambo ambalo ukweli unaweza kupata msaada. Kuna mambo mengi unayofikiria hayana majibu lakini ukweli ni kuwa yana majibu kama ukiamua kutafuta msaada