Category: Uncategorized

  • Tafakari ya kufikirisha 44/366-2024

    Uongozi wa kujitambua unahusisha kiongozi kupenda zaidi kujifunza kuliko kuamini yupo sahihi mara zote. Huu ni mtego mbaya kwenye Uongozi, kwa sababu watu wa chini hawataki kukuudhi, wanaweza kuona makosa unayofanya lakini wasikuambie, kama Kiongozi una tabia ya kuamia uko sahihi mara zote nukuu toka kwa Dr. Makirita Amani

  • Tafakari ya kufikirisha 43/366-2024

    Mara zote kuwa na mtazamo wa mwanafunzi, usijione mkubwa kushindwa kuuliza maswali, kamwe usijione unajua sana ili uweze kujifunza kitu kipya mara zote hii itakusaidia kuongeza maarifa mengi zaidi na kuwa tayari kujifunza mara zote.

  • Tafakari ya kufikirisha 41/366-2024

    Watu wengi wanaoshindwa siyo kwa sababu hawana uwezo au akili lakini wanashindwa kwa sababu ya kukosa kuamua,uelekeo,kujitoa na , nidhamu Nukuu toka kwa Shiv Khera ambapo mwandishi anakwenda kinyume na dhana za kwenye jamii kwamba watu waliofanikiwa lazima wawe na akili au uwezo fulani mkubwa ndio wapate mafanikio bali lazima kuwa na vitu vingine vya…

  • Tafakari ya kufikirisha 40/366-2024

    Lengo kuu la kuanzisha biashara ni kuwa na mwendelezo, kuwa na chanzo cha uhakika cha mzunguko wa fedha ili kuzidi au kukidhi gharama na matumizi ili baadae uweze kuzishikilia fedha nukuu toka kwa mwandishi Brian Tracy Mtaalamu wa masuala ya Uongozi , hapa tunapata funzo kubwa kwenye biashara kwamba ni kitu ambacho kinafanya muendelezo wa…

  • Tafakari ya kufikirisha 39/366-2024

    Moja ya changamoto ya wasiwasi ambao unapelekea magumu unatokana na kutotambua tatizo mapema kabisa kabla halijatokea, hivyo kupitia kutambua tatizo mapema kunakusaidia katika kuepuka na changamoto na kukabiliana na hatari ambazo zinaweza kumtokea mtu kabla hajakutana na changamoto kubwa.

  • Tafakari ya kufirikisha 38/366-2024

    Mahusiano ndio kila kitu. Kila kitu ulimwenguni ambacho ni kwa sababu ya kinahusiana na kitu kingine.Hakuna kitu ambacho kipo kwa kujitegemea chenyewe. Tunatakiwa kuacha kuigiza kwamba tutakwenda navyo peke yetu nukuu toka kwa Margaret Wheatley, tafakari hii inatupa hamasa kwamba vitu …ambavyo tunafanya mara zote tukifanya kwa ushirikiano tutapata mafanikio makubwa zaidi kuliko tukifanya peke…

  • Tafakari ya kufikirisha 37/366-2024

    Mafanikio kwenye maisha hayaamuliwi na kitu gani tunafanya kulinganisha na watu wengine, bali ni kulinganisha kile ambacho tunafanya na kile ambacho tungepaswa kufanya kutokana na uwezo wetu hayo ndio mafanikio ambayo yanazungumziwa by Shiv Khera

  • Tafakari ya kufikirisha 36/366-2024

    Matatizo mengi ambayo yanatukabili hayatokani na kutokujua nini cha kufanya bali yanatokana na kutokufanya kile ambacho tunakijua, ni nani asije ukifanya mazoezi unajenga mwili na kuongeaza kinga ya mwili, nani asiyejua ulevi na uvutaji wa sigara una madhara lakini ndio vitu ambavyo vinafanywa kwa kiasi kikubwa.

  • Tafakari ya kufikirisha 34/366-2024

    Kuna njia moja tu kuweza kumshawishi mtu kufanya kitu chochote kile. Njia hiyo ni kumfanya mtu huyo atake kufanya kitu hicho yeye mwenyewe bila kulazimishwa nukuu toka kwa Dargi Cargie. Hapa mwandishi anazungumzia kwamba chochote ambacho mtu anaweza kufanya ni lazima ndani yake na huo ndio ushindi mkuu katika kuchukua hatua.

  • Tafakari ya kufikirisha 33/366-2024

    Watu hudhani wanahitaji maandalizi makubwa sana ndiyo waweze kuanza kufanya. Huona kutakuwa na vikwazo vingi kwenye ufanyaji hivyo kujipanga zaidi ili waweze kuvivuka. Lakini ukweli ni kwamba kile wanachofikiria sivyo uhalisia ulivyo. Ndiyo maana wengi wanaojisukuma na wakaanza kufanya huwa ni rahisi kwao kuendelea kufanya. Hivyo ni kwa sababu uhalisia waliokutana nao unakuwa tofauti na…