Category: Uncategorized

  • Tafakari ya kufikirisha 54/366-2024

    Kujiamini kunakujengea kujithamini na kujithamini ndio kunakusukuma kufanya mambo ambayo ni bora na muhimu kwako. Hii inaongeza ufanisi kwenye jambo lolote unalofanya na hivyo kukuhakikishia ushindi.Unapoamini kwamba unaweza kushinda,unageuza changamoto zozote unazokutana nazo kuwa sehemu ya ushindi wako. Unapofika wakati na kuona hakuna njia tena ya kwenda mbele,imani yake pekee ndio itakayokuvusha hapo.Kuamini kwamba unaweza…

  • Tafakari ya kufikirisha 53/366-2024

    Kama utaishi muda mrefu lazima utafanya makosa.Lakini kama utajifunza kutokana na makosa utakuwa mtu bora.Ni jinsi gani unakabiliana na matatizo na siyo jinsi gani yanakuathiri. Kitu kikubwa ni kutokata tamaa, kutokata tamaa kutokata tamaa

  • Tafakari ya kufikirisha 52/366-2024

    Ushindi tunaoutaka kwenye maisha siyo kama mbio ambapo mmoja akishinda wengine wote hamna tena nafasi ya kushinda kwenye mbio hizo mlizoshiriki kwa wakati huu. Ushindi wetu kwenye maisha ni mbio nyingi ambazo kila mmoja wetu anajua anakimbia kuelekea wapi. Katika mbio hizi nyingi ndio kila mmoja wetu anaweza kushindana na uwezo wake na utofauti wake

  • Tafakari ya kufikirisha 51/366-2024

    Kadri ambavyo unaona jambo liko just ya uwezo wake na hauwezi kulitatua ndivyo ambavyo utazidi kujiona hauna thamani na utaendelea kukata tamaa. Usikubal kuendelea kutatizwa na jambo ambalo ukweli unaweza kupata msaada. Kuna mambo me mengi unayofikiria hayana majibu lakini ukweli ni kuwa yana majibu kama ukiamua kutafuna majibu.

  • Tafakari ya kufikirisha 50/366-2024

    Maono sahihi yanayochangiwa na mipango sahihi iliyonyooka yanakupa hamasa kubwa, hisia na nguvu binafsi kubwa katika kufikia mafanikio makubwa. Kwa kutumia nguvu ya mipango iliyonyooka inakusaidia kupata nguvu katika kutimiza maono yako makubwa na mipango kwenye maisha na kufikisha malengo Mhamasishaji Brian Tracy anatusisitiza katika mafundisho yake hayo kwenye maisha.

  • Tafakari ya kufikirisha 49/366-2024

    Haijalishi unapitia nini,jua muda ni mwalimu na tiba nzuri.Kadiri muda unavyokwenda mambo hayo yatabadilika,au yataondoka kabisa. Na kama hayataondoka ,basi wewe utaondoka na kuyaacha. Je kuna haja ya wewe kusumbuka na chochote ili hali mabadiliko yatakuja? Kuna haja ya wewe kukata tamaa wakati hakuna kinachobaki vili kilivyo milele? Ni dhahiri kwamba yote hayo hayana haja,wajibu…

  • Tafakari ya kufikirisha 48/366-2024

    Mafanikio makubwa mara zote yanatokana na kujiandaa na kupambana na maumivu, ndio maana mara nyingi watu waliofanikiwa wengi maisha wanayoishi baada ya kufanikiwa ni tofauti na kabla ya kufanikiwa ukifuatilia nyuma ya pazia kuna maumivu ambayo walipitia au walijiandaa kukabiliana nayo lakini picha baada ya kufanikiwa ndio inaonekana kuliko kabla ya kufanikiwa

  • Tafakari ya kufikirisha 47/366-2024

    Sisi ni zao la kile ambacho tunakirudiarudia kufanya,Ubora siyo kufanya bali ni kurudiakurudia ndio maana ukifanya jambo fulani mara kwa mara hata kwenye jamii watu watakuita kwa jina hilo kwa sababu utakuwa umeona ubora kwenye kitu hicho hivyo kwa chochote unachofanya jua ubora upo kwenye kurudiarudia na siyo kufanya mara moja ndio maana ukiwa unafanya…

  • Tafakari ya kufikirisha 46/366-2024

    Kushindwa kwingi kwenye maisha kunatokana na watu ambao hawajatambua jinsi gani walivyokuwa karibu na mafanikio pale ambapo wanakata tamaa na kuacha kufanya jambo au kitu ambacho walikuwa wanafanya nukuu toka kwa Mgunduzi Thomas Edson

  • Tafakari ya kufikirisha 45/366-2024

    Ugumu unauona kabla ya kuanza kitu huwa tofauti kabisa na uhalisia wa baada ya kuanza kufanya.Kinachoonekana kutokuwezekana kabisa kabla ya kuanza,kinawezekana baada ya kuanza. Anza kufanya kila unachopanga, tena anza kufanya ukiwa na moto wa kupanga.Usijali sana utaendeleaje, kwa sababu utalivuka daraja pale unapolifikia.Anza na kukabiliana na kila linalokuja mbele yako. Hivyo ndio njia ya…