Category: Uncategorized

  • Tafakari ya kufikirisha 76/366-2024

    Kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kupita mbele ya macho yako, lakini kuna vichache ambavyo vinaweza kugusa moyo wako. Vile ambavyo vitakugusa ndio unavyopaswa kuchukua hatua kuvifanya kwa sababu hatua zinachangiwa na hisia Mwandishi John Maxwell ameiongelea kwa kina kwenye kitabu chake chake Kipaji Pekee hakitoshi.

  • Tafakari ya kufikirisha 75/366-2024

    Linapokuja suala la kuchukua hatua au msukumo kuna aina nne za watu i) Watu wanaofanya jambo sahihi bila ya kuambiwa 2) Watu wanaofanya jambo sahihi baada ya kuambiwa 3) Watu wanaofanya jambo sahihi baada ya kuambiwa zaidi ya mara moja 4) Watu ambao hawafanyi jambo sahihi, haijalishi mazingira yoyote yale. Mwandishi John Maxwell kwenye kitabu…

  • Tafakari ya kufikirisha 74/366-2024

    Hatuwezi kuwa vile ambavyo tunataka kwa kuwa vile ambavyo tupo sasa hivi , kwa chochote ambacho tunataka kukibadili zaidi ya tulivyo sasa lazima tuchukue hatua zaidi kwa vitendo ambavyo mara zote lazima vitahusisha kufanya au kutoka pale ulipo ili kuwa bora zaidi hauwezi kupunguxa uzito kama unataka kuendelea kula kila mlo kama imeandikwa kwenye katiba…

  • Tafakari ya kufikirisha 73/366-2024

    Tabia moja ambayo inafanana na ipo kwa waliofanikiwa ni kwamba wamevuka au hawana tabia ya kukata tamaa, ndio maana wanaweza kukatishwa tamaa lakini wakaendelea kufanya yale ambayo wamepanga kufanya bila kusubiri maoni ya watu hivyo mara zote ukiwa unafanya jambo endelea kufanya bila ya kusubiri maoni ya watu ili kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha…

  • Tafakari ya kufikirisha 70/366-2024

    Hakuna mtu anayepata mafanikio kwa kufanya kila kitu ambacho anatakiwa kufanya pekee. Kiwango cha mbele zaidi ya kile ambacho unapaswa au unatakiwa kufanya ndio inawakilisha ubora kwa maana chochote ambavyo unafanya kwa juhudi za ziada kinaashiria ubora na mafanikio zaidi.

  • Tafakari ya kufikirisha 69/366-2024

    Usiogope kuweka nguvu kwenye kile kitu kinachoonekana ni kazi ndogo.Mara zote unavyozidi kufanya weka nguvu kubwa zaidi ili uzidi kuimarika na kuchukua hatua nukuu toka kwa Dan Carginie

  • Tafakari ya kufikirisha 68/366-2024

    Muda mwingi ambao unapotea ni muda wa kujiandaa kuanza, na hapo ndipo ambapo panawafanya watu kuchelewa kuchukua hatua kwenye maisha kwa kiasi kikubwa na kujikuta hawajaanza mara zote.

  • Tafakari ya kufikirisha 67/366-2024

    Kama unataka kushindwa amini kwenye bahati.Kama unataka kufanikiwa amini kwenye kanuni za vitendo na matokeo, hapo utajingenezea bahati yako binafsi nukuu toka kwa Shiv Khera, Mwandishi anatusisitiza kwamba bahati inatokana na kuchukua hatua na siyo kitu kingine chochote.

  • Tafakari ya kufikirisha 66/366-2024

    Njia bora ya kuifanya kesho yako kuwa bora ni kujua kitu gani kibaya ambacho umekifanya Leo na kujifanyia tathmini kwenye yale uliyoyafanya ili uweze kufanya kwa ubora zaidi siku inayofuata mwandishi nguli Robin Sharma anasisitiza zaidi katika kufanya tathmini kwa kila siku ambayo unaimaliza na hii itapelekea kuwa na siku nyingine bora zaidi.

  • Tafakari y kufikirisha 65/366-2024

    Sababu kuu ya wale wanaoshindwa kufanya makubwa kwenye muda walionao ni yale wanayochagua kufanya kwenye muda huo.Wanaoshindwa kufanya makubwa wanatumia muda wao kufanya mambo yasiyokuwa na tija. Kwa maneno mengine wanatumia muda huo kuhangaika na usumbufu badala ya kuhangaika yale yenye tija ambayo ambayo yatachangia mtu kupiga hatua zaidi kwenye maisha yao nukuu toka kwa…