Category: Uncategorized
-
Tafakari ya kufikirisha 211/366-2024
Pale tunapoona kushindwa ni kitu ambacho kinaweza kutokea wakati tunapiga hatua, hakuna haja ya kuogopa ya kushindwa. Tunaweza kuangalia kushindwa kama sehemu nyingine ya kujaribu, na hali ambayo inaweza kuwa ina majibu kwenye mafanikio yanayokuja.
-
Tafakari ya kufikirisha 210/306-2024
Watu wengi hawaombi ushauri bali wanataka kusikia kile ambacho kipo ndani yao, ndio maana mtu anaweza kuja kuomba ushauri lakini hakakuambia kwamba umempa ushauri mbaya ni kwa sababu haujahalarisha kile ambacho anakitaka yeye unapoomba ushauri lazima uwe tayari kubadilika na siyo kutaka kuhalarisha kile unachokitaka wewe Mwanafalsafa Epictetus anatushikisha jambo hili.
-
Tafakari ya kufikirisha 209/366-2024
Ukiwa unafikiria au kuwa na hofu andika kile ambacho unakiohofia na utaona yale ambayo yatatokea baada ya muda, yanaweza yasiwe na athari kama vile ulivyokuwa unahofia Mwanafalsafa Epictetus anatushikisha jambo hili.
-
Tafakari ya kufikirisha 208/366-2024
Kama unataka kuboresha maisha yako na kuishi kwenye yale unayostahili, lazima ukimbie mbio zako mwenyewe. Haijalishi watu wengine watasemaje.Kitu muhimu ni kile unachojiambia mwenyewe, kujisikia huru ndani yako.Kuwa mkweli ndani yako. Hicho ndio chanzo kikuu cha Furaha.
-
Tafakari ya kufikirisha 207/366-2024
Kuna watu wanajifunza kutokana na makosa ambayo yamefanywa na watu wengine. Ni watu wenye hekima. Watu wengine wanafikiri uzoefu wa kweli unatokana na uzoefu wa mtu binafsi. Kuna watu wanavumilia maumivu na masononeko yasiyohitajika kwenye maisha yao yote kwa kutotaka kujifunza kwa wengine.Maandishi ni moja ya sehemu mojawapo ya kujifunza makosa yaliyofanywa na watu wengine…
-
Tafakari ya kufikirisha 206/366-2024
Hakuna kukosea kwenye maisha bali ni somo.Hakuna hicho kitu kinachoitwa uzoefu hasi, bali ni fursa ya kukua, kujifunza na kupanda kwenye njia ya udhibiti binafsi. Hata maumivu yanaweza kuwa Mwalimu bora sana.
-
Tafakari ya kufikirisha 205/366-2024
Kila mmoja wetu ana upande wa giza na upande wa mwanga. Kila mmoja wetu kuna mapungufu ya kurekebisha na majeraha ya kuyaonyesha ili kuyaponya. Kila upande wa mtu kuna nyakati alikuwa na moyo ulioumia. Hali hii ya mapungufu ndio unaleta na kufanya hali ya ubinadamu Mwandishi Robin Sharma anatushirikisha jambo hili.
-
Tafakari ya kufikirisha 204/366-2024
Kwenye maisha vitu vidogo ndio vitu vikubwa. Na ubora wa maisha ambao utakutana nao unatokana na vitu vidogo vidogo ambavyo utachagua kwenye kila dakika ya kila saa kwenye kila siku yako .
-
Tafakari ya kufikirisha 203/366-2024
2 Toka kwenye mazoea au eneo ambalo una mazoea nalo.Utapata ukuaji kama uko tayari unauwoga na haujisikii vizuri wakati unajaribu vitu vipya mwandishi Brian Tracy anatushirikisha jambo hili.
-
Tafakari ya kufikirisha 202/366-2024
Matatizo mengi madogo madogo kwenye maisha ambayo yanatusumbua sana yapo chini ya shilingi milioni moja.Ndio maana mara nyingi watu wamekuwa wakikopa pesa ndogo chini ya millioni moja ili kukabiliana na changamoto za dharura ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara na hivyo kupelekea changamoto za madeni kuzidi kujitokeza kwenye maisha” mfano fuatilia mikopo mingi ya mtandaoni…