Tafakari ya kufikirisha 25/366 -2024

Msukumo unaotoka ndani ya mtu ndio unaomfanya mtu kuchukua hatua mara moja kwenye kila linalotokea, bila ya kusubiri kwa muda mrefu. Wenye msukumo wa ndani hawasubiri mpaka wapate taarifa zaidi na kujadiliana na wengine ndiyo wachukue hatua.Wao huchukua hatua mara moja pale inapohitajika kufanya hivyo, bila ya kusitasita. Ni msukumo huo wa kuchukua hatua na kufanya hivyo ndiyo unaowatofautisha wanaopata mafanikio makubwa na wanaoishia kupata mafanikio madogo. Kitu cha kujiuliza kwa upande wako unavyofanya jambo msukumo unaanzia wapi ndani yako au nje yako.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *