Habari Rafiki utakubaliana na mimi kwenye jamii zetu ambayo inatuzunguka matatizo mengi ambayo yanatusumbua ni yale madogo ambayo yapo chini ya kiwango cha Shilingi Milioni Moja. Angalia watu ambao wanakuomba mara nyingi kiwango gani cha fedha ambacho wanakuwa wanakiomba utakuja kuona kwa kiasi kikubwa kiasi hicho kwenye mzunguko wa chini ya shilingi Milioni Moja.
Fuatilia Hata taasisi za ukopeshaji za mtaani na Vicoba pamoja mifumo ya ukopeshaji ya mtandaoni inayojiendesha na kutoa mikopo midogo mingi ipo chini ya Milioni Moja, kwa nini? kwasababu wamegundua ndipo ambapo kuna fursa imejificha ndani yake ya tatizo.
Hivyo amua sasa kutengeneza mpango wa kuweka akiba kidogo kidogo ili uweze kufikia kiwango hiki ambacho unaweza kukiweka kwenye akaunti maalumu au ukaweka nyumbani na kukitunza kwenye sehemu ambayo hauwezi kuchukua kwa urahisi.
Habari Njema ni kwamba kwenye kitabu cha JILIPE MWENYEWE KWANZA tumekupa sababu Hamsini ambazo unaweza kuzitumia kuwa chachu ya wewe kuweza kufikia malengo ya kujiwekea akiba na kutimiza majukumu ya dharura ambapo yanaweza kujitokeza na pia tumekupa sehemu unaweza kuweka kiasi kile cha fedha ambacho utakitumia kujilipa wewe Mwenyewe kwanza ili kufikia malengo yako ambayo umejiwekea katika maisha.
Kitabu hiki kinapatikana kwa Nakala Ngumu kwa bei ya ofa shs 20000 au unaweza kukipata kwa Nakala Laini kupitia link https://vitabu.somavitabu.co.tz/#/view/shop-item/98/
Leave a Reply