Tafakari ya kufikirisha 71/365-2025

Ukianza kujishika na vitu, watu au fedha ndiyo unavuruga kila kitu Dhumuni la maisha ní
ní kuthamini kila kitu na kutokujishika na chochote. Ukishaanza kusema hiki ní changu nastahili kuwa nacho wakati wote, iwe ní fedha, vitu au watu, ndipo mambo yanapokuwa magumu. Ukianza kusema ílí niwe na furaha lazima niwe na kitu fulani au Kiasi fulani cha fedha au niwe na watu fulani, jua kabisa kwamba hutaweza kuwa na furaha. Thamini kila kitu unachokutana nacho kwenye maisha, kitumie kwa wakati unacho na jua wakati wowote kinaweza kuondoka. Usijishike au kung’ang’ana na vitu. Pia jifunze kutoa kwa wengine, hii itakusaidia kutojishika na vitu pia itafungua milango ya kupata zaidi Nukuu toka kwa Andrew Mathew


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *