Tafakari ya kufikirisha 14/366-2024

Jambo moja la kushangaza kuhusu sisi binadamu ni hili, tupo tayari kumpa kila mtu mudawetu ila hatupo tayari kujipa muda huo sisi wenyewe, Mtu ataamka asubuhi na haraka sana anakimbilia kwenye mitandao na kupata habari, akitoka hapo anakutana na wengine ambazo wataanza kumweleza mambo mbalimbali ambayo hata siyo muhimu kwake. Atatumia kubishana kuhusu michezo, siasa na mengine, lakini hawezi kupata dakika chache za kukaa yeye kama yeye. Tumekuwa tunajinyima fursa muhimu sana kwenye maisha yetu, tumekuwa tunawapa wengine zawadi hii muhimu ya muda lakini tunajisahau sisi wenyewe kitu ambacho kinapelekea msongo wa mawazo na kukata tamaa nukuu toka kitabu cha pata masaa mawili ya ziada kilichoandikwa na Dr. Makirita Amani


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *