Tafakari ya Kufikirisha 167/366-2024

Sisi binadamu tunasukumwa na hisia kuu mbili,tamaa ya kupata na hofu ya kupoteza.Lakini nguvu ya hisia hizo hazilingani, hofu ya kupoteza ina msukumo mkubwa kuliko tamaa ya kupata. Mfano kama ukiambiwa kukamilisha jukumu fulani utaongezwa laki moja utajisukuma kufanya lakini ukishindwa hutaumia sana. Lakini ukiambiwa usipokamilisha jukumu hilo utakatwa laki moja,hapo utapambana uwezavyo. Kupoteza laki moja kunaumiza kuliko raha unayoipata kwa kupata laki moja hiyo hiyo.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *