Tafakari ya kufikirisha 49/366-2024

Haijalishi unapitia nini,jua muda ni mwalimu na tiba nzuri.Kadiri muda unavyokwenda mambo hayo yatabadilika,au yataondoka kabisa. Na kama hayataondoka ,basi wewe utaondoka na kuyaacha. Je kuna haja ya wewe kusumbuka na chochote ili hali mabadiliko yatakuja? Kuna haja ya wewe kukata tamaa wakati hakuna kinachobaki vili kilivyo milele? Ni dhahiri kwamba yote hayo hayana haja,wajibu wako ni kukabiliana na yale unayokutana nayo kwa namna sahihi ukijua hayatadumu milele. Kamwe usikate tamaa na kuona chochote unachokutana nacho ndiyo mwisho,kila kitu kinabadilika , anza kwa wewe kubadilika na kuwa tayari kupokea mabadiliko ya vitu vingine ili kunufaika nayo nukuu toka kwa nguli wa Falsafa Marcus Aurelius


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *