MIAKA MITANO MAMBO MATANO AMBAYO NIMEJIFUNZA TANGU KUTOA WAZO LA KUANZISHA MKOBA/SACCOS KWENYE VIKUNDI VYOTE VYA SHULE NILIZOSOMA MWAKA 2019.
- MATATIZO YAPO PALEPALE;
Ndio wakati natoa wazo hili niliona changamoto ya kuchangishana fedha kama za misiba au Ugonjwa vitu ambavyo ni dharura ambazo zinaweza kumtokea mtu yeyote kwa sababu kila kitu ambacho tuko nacho tumepewa kwa muda na pale vikitakiwa vitachukuliwa zilipokuwa zinasumbua kudaina na kuchukua muda mrefu na hivyo kuchelewa kusaidia walenga kutatua matatizo husika ya dharura kwa wakati. Lakini na tangu hapo matatizo bado yameendelea kutokea na watu kutaka kuendelea kuchangishana michango ya vitu ambavyo vipo na wanajua vinaweza kutokea.Wakati mwingine kulaumu wengine.
- ELIMU YA JUU SIYO KIGEZO CHA WATU KUCHUKUA HATUA;
Wakati natoa wazo lile nilikuwa nafikiri watu ambao ambao wamesoma mpaka Elimu ya juu wanaweza kuchukua hatua kwa haraka na kuweza kufanya kitu kikubwa lakini mwitikio ulikuwa vilevile sawasawa na makundi ambayo yana watu ambao wameishia kuwa na elimu chini ya kiwango cha kati kulinganisha na Elimu ya juu, kwa upande mwingine ndipo kwenye tofauti kati ya Elimu na Hekima ni kuchukua hatua.
- MUDA UKIKUACHA UNAWEZA KULAUMU WATU KWA SABABU YA UZEMBE WAKO WA KUTOCHUKUA HATUA KWA WAKATI NA KUPUUZA:
Moja ya kitu ambacho kilikuja kujitokeza baada ya watu kuanza hivi vikundi vya Mkoba na kuanza kuchanga kuna ambao walipata matatizo miaka miwili au mitatu mbele ambapo waliambiwa ili watimize vigezo hivi walipaswa kutoa michango yote ya nyuma ambapo kwa muda umemshapita mtu aliona anatoa fedha nyingi kwa wakati mmoja lakini , mwanzoni watu walikuwa wanatoa hata elfu moja moja na kufikisha kiwango cha elfu 10000 kwa mwezi. Huu ndio ule uthibitisho wa kauli muda ni mali unavyofanya kazi
- MATATIZO YANAWEZA KUKUTOKEA KWA PALE AMBAPO HAUKUTARAJIA:
Ndio kwa kiasi kikubwa watu ambao walipuuza au kutoona umuhimu wa makundi haya ya ushirikiano pasipotarajiwa baadhi zimewakuta changamoto na kupelekea wengine kutamani wawachangie au kulaumu watu na kuona kama wanafanyiwa ubaya lakini ukiangalia kadri muda unavyozidi kwenda watu wanakuwa na ongezeko la majukumu hivyo na kupelekea nyakati fulani mwitikio kuwa mdogo kwa sababu ya nyakati husika ambazo mtu anaweza kuwa amepatwa na changamoto.
- MICHANGO HII INAWEZA KUWA FURSA KUBWA YA MITAJI HUKO MBELENI;
Mwanzoni wakati makusanyo ya michango hii ya vikundi yanaanza ilikuwa inachukuliwa kama kitu kidogo lakini kadri watu wanavyoendelea kukusanya wamejikuta wakiwa na kiwango kikubwa cha fedha ambacho , vikundi vingine vimeanza mipango ya kuwekeza hata kwenye Hati fungani kama hii ya SAMIA Infrastructure Bond na ukawa sehemu ya Wajenga Barabara za Nchi hii badala ya kulaumu Barabara mbovu za mtaani kwako mara zote na unakuwa umetoa mchango kwa Nchi na huku ukipata faida, unaweza kukuta hiyo faida ikatumika kukatia pia bima za afya kwa wanachama wote na kuwapa Faraja wanachama ni kitu ambacho ni kizuri kitasaidia wanachama ambao hawana hizo Bima kunufaika kama wale wanakijiji wa Njombe wanavyofaidika na kuchukua hatua huku wasomi wakipiga soga na kushindwa hatua hata ndogo tu.
Rafiki hayo ndio mambo Matano ambayo nimeyakusanya na kujifunza unaweza kushirikisha nawe uzoefu na faida za Mkoba/Saccoss za kwenye shule ambazo umesoma na umeona manufaa yake ambayo umepata kuwepo kwenye vikundi hivyo kwa sababu shule hazibadiliki ulizosoma hivyo mnaweza kufanya vitu kwenye vitu hivyo kwa kutumia vikundi hivyo vya kudumu kama shule.
Eng. Tindwa Martin
Mwandishi wa Kitabu JILIPE MWENYEWE KWANZA
Leave a Reply