Tafakari ya kufikirisha 178/366-2024

Kimbia mbio zako mwenyewe, Hakuna watu wawili ambao wanafanana kwa kila kitu hapa duniani.Hata mapacha wa kufanana,bado hawafanani kwa kila kitu.Hivyo ulivyo wewe, ni toleo pekee ambalo limewahi kuwepo hapa duniani na hakutakuja kuwa na toleo jingine kama lako. Lakini jamii imekupotosha,imekuwa inakufananisha,kukulinganisha na kukushindanisha na wengine kitu ambacho kimepelekea wewe kushindwa kutambua upekee wako na kuweza kuuishi.Ukiwa shuleni unapewa mtihani mmoja na wengine na mnashindanishwa kama vile mnalingana kwa kila kitu.Ukiwa kazini,ufanisi wako unalinganishwa na wengine. Kadhalika kwenye jamii,maisha yako yanalinganishwa na kupimwa na wengine Tafakari toka kitabu cha Mwongozo wa Maisha ya Mafanikio cha Dr. Makirita Amani


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *