Linapokuja suala la kuchukua hatua au msukumo kuna aina nne za watu i) Watu wanaofanya jambo sahihi bila ya kuambiwa 2) Watu wanaofanya jambo sahihi baada ya kuambiwa 3) Watu wanaofanya jambo sahihi baada ya kuambiwa zaidi ya mara moja 4) Watu ambao hawafanyi jambo sahihi, haijalishi mazingira yoyote yale. Mwandishi John Maxwell kwenye kitabu chake cha Kipaji pekee hakitoshi anasema Kwa mtu yoyote ambaye anataka kufanyia kazi kipaji zaidi lazima awe katika kundi namba moja, kwa nini kila mmoja haangukii kwenye kundi hilo anasema kila mtu ana sababu zake, kwa hiyo chochote unachofanya angalia sababu zako za kukufanya kuangukia kwenye kundi mojawapo. Kwa chochote unachofanya angalia kundi ambalo unaangukia na sababu ambazo umechagua kwenye kufanya kitu hicho.
Tafakari ya kufikirisha 75/366-2024
by
Tags:
Leave a Reply