Kujiamini kunakujengea kujithamini na kujithamini ndio kunakusukuma kufanya mambo ambayo ni bora na muhimu kwako. Hii inaongeza ufanisi kwenye jambo lolote unalofanya na hivyo kukuhakikishia ushindi.Unapoamini kwamba unaweza kushinda,unageuza changamoto zozote unazokutana nazo kuwa sehemu ya ushindi wako. Unapofika wakati na kuona hakuna njia tena ya kwenda mbele,imani yake pekee ndio itakayokuvusha hapo.Kuamini kwamba unaweza kushinda ni muhimu sana ili wewe uweze kushinda kwenye maisha yako.
Tafakari ya kufikirisha 54/366-2024
by
Tags:
Leave a Reply