Usitamani watu wawe tofauti bali tamani wajidhihirishe mapema. Usitamani watu wawe vile unavyotaka wewe, bali tamani kuujua uhalisia wao. Ni pale watu wanapokuonyesha uhalisia wao usiwakatalie kutaka wawe tofauti wala usiumie kwa sababu ulitaka wawe tofauti. Unachopaswa ni kupima, kwa uhalisia ambao unaujua kuhusu watu, je bado unaweza kwenda pamoja na kila mtu akanufaika.
Tafakari ya kufikirisha 30/366-2024
by
Tags:
Leave a Reply