Msukumo unaotoka n dani ya mtu ndio unaomfanya mtu kuchukua hatua mara moja kwenye kila linalotokea, bila ya kusubirii kwa muda mrefu. Wenye msukumo wa ndani hawasubiri mpaka wapate taarifa zaidi na kujadiliana na wengine ndiyo wachukue hatua. Wao huchukua hatua mara moja pale inapohitajika kufanya hivyo, bila ya kusitasita. Ni msukumo huo wa kuchukua hatua na kufanya ndiyo unaowatofautisha wanaopata mafanikio makubwa na wanaishia kupata mafanikio madogo.Kitu cha kujiuliza kwa upande wako unavyofanya jambo msukumo unaanzia wapi ndani yako au nje yako.
Tafakari ya kufikirisha 24/366
by
Tags:
Leave a Reply